+ -

عن عبد الله بنِ عمر رضي الله عنهما أن عمرَ بْن الخطاب رضي الله عنه قال: ((يا رسول الله، أّيَرقُدُ أَحَدُنا وهو جُنُب؟ قال: نعم، إِذَا تَوَضَّأ أَحَدُكُم فَليَرقُد)).
[صحيح] - [متفق عليه]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abdillahi bin Omar -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- Yakwamba Omar bin Khattwab -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Alisema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu Je anaweza kulala mmoja wetu akiwa na janaba? Akasema: "Ndiyo, atakapotawadha mmoja wenu basi na alale"
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim]

Ufafanuzi

Alimuuliza Omar bin Khattwab -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- ikiwa mmoja wao atapatwa na janaba mwanzoni mwa usiku, kwa kumuingilia mke wake hata kama hakumwaga au akajiotea, Je alale nayeye akiwa na janaba? Akawaruhusu -Rehema na Amani ziwe juu yake- kwa hilo, kwa kupunguza hadathi (uchafu) huu mkubwa kwa udhu wa kisheria; na hapo haina tatizo mtu kulala na janaba.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo
Kuonyesha Tarjama