عَنْ عَائِشَةَ أُمِّ المُؤمنينَ رضي الله عنها قَالَتْ:
كَانَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يُعْجِبُهُ التَّيَمُّنُ، فِي تَنَعُّلِهِ، وَتَرَجُّلِهِ، وَطُهُورِهِ، وَفِي شَأْنِهِ كُلِّهِ.
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 168]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake amesema:
Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akipendezwa sana na kuanzia kulia, katika kuvaa kwake viatu, na kutana kwake nywele, na twahara yake, na katika mambo yake yote.
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 168]
Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa akipenda na akipendelea kuanza na upande wa kulia katika mambo yake yanayostahiki heshima, na miongoni mwake ni: Kuanza na mguu wa kulia katika kuvaa viatu vyake, na kuanzia kulia katika kutana nywele za kichwa chake, kuziachanisha kwake na kuzipaka kwake mafuta, na katika kutawadha kwake, anatanguliza kulia kabla ya kushoto katika mikono na miguu.