عَنِ الْبَرَاءِ رَضيَ اللهُ عنه قَالَ:
مَا رَأَيْتُ مِنْ ذِي لِمَّةٍ أَحْسَنَ فِي حُلَّةٍ حَمْرَاءَ مِنْ رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، شَعْرُهُ يَضْرِبُ مَنْكِبَيْهِ، بَعِيدَ مَا بَيْنَ الْمَنْكِبَيْنِ، لَيْسَ بِالطَّوِيلِ وَلَا بِالْقَصِيرِ.
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح مسلم: 2337]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Baraa -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema:
Sijawahi kumuona mwenye nywele ndefu na vazi jekundu zuri kuliko Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake, nywele zake zinapigapiga mabega yake, na mabega yake yako mbali mbali, si mrefu wala mfupi.
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح مسلم - 2337]
Anaeleza Baraa bin Azibi radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake ya kwamba hajawahi kumuona yeyote nywele za kichwa chake ni ndefu zimefika katika mabega yake, na anayevaa kikoi na shuka jeusi na lenye mistari myekundu zuri kuliko Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake, na kwamba miongoni mwa sifa zake za kimaumbile ni kwamba mabega yake yalikuwa mbali mbali, mwenye kifua kipana, na alikuwa na kimo cha kati na kati, kati mrefu na mfupi.