+ -

عَنْ ابنِ عُمَرَ رَضيَ اللهُ عنهما عَنْ رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:
«مَنِ اقْتَنَى كَلْبًا إِلَّا كَلْبَ ضَارٍ أَوْ مَاشِيَةٍ نَقَصَ مِنْ عَمَلِهِ كُلَّ يَوْمٍ قِيرَاطَانِ»، قَالَ سَالِمٌ: وَكَانَ أَبُو هُرَيْرَةَ يَقُولُ: «أَوْ كَلْبَ حَرْثٍ»، وَكَانَ صَاحِبَ حَرْثٍ.

[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح مسلم: 1574]
المزيــد ...

Na imepokelewa kutoka kwa bin Omari -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake yeye na baba yake -kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake- amesema:
"Atakayefuga mbwa isipokuwa mbwa wa mawindo au wa mifugo, basi yatapungua katika matendo yake kila siku kiratu (shehena) mbili", Amesema Salim: Na alikuwa Abuu Huraira akisema: "Au mbwa wa shamba", Naye akawa na shamba.

[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح مسلم - 1574]

Ufafanuzi

Ametahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kufuga mbwa, isipokuwa kwa haja ya kuwinda, au kulinda mifugo na mazao, na atakayemfuga pasina haja hizo zitapungua katika thawabu za matendo yake kila siku shehena mbili; ambazo ujazo wake unajulikana mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kiassam الأمهرية الهولندية الغوجاراتية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Hifai kwa muislamu kufuga mbwa, isipokuwa katika hali zilizotajwa.
  2. Kukatazwa kufuga mbwa; kwa sababu ya hasara na madhara mengi yanayopatikana ndani yake, kwani imethibiti kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa Malaika hawaingii nyumba ambayo kuna mbwa ndani yake; na ni kwa sababu mbwa ananajisi nzito ambayo hakuna kinachoweza kuiondosha isipokuwa kurudiarudia kuosha kwa maji na udongo.