+ -

عَنْ ‌أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ:
أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ افْتَقَدَ ثَابِتَ بْنَ قَيْسٍ، فَقَالَ رَجُلٌ: يَا رَسُولَ اللهِ، أَنَا أَعْلَمُ لَكَ عِلْمَهُ، فَأَتَاهُ فَوَجَدَهُ جَالِسًا فِي بَيْتِهِ، مُنَكِّسًا رَأْسَهُ، فَقَالَ: مَا شَأْنُكَ؟ فَقَالَ شَرٌّ، كَانَ يَرْفَعُ صَوْتَهُ فَوْقَ صَوْتِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَدْ حَبِطَ عَمَلُهُ، وَهُوَ مِنْ أَهْلِ النَّارِ، فَأَتَى الرَّجُلُ فَأَخْبَرَهُ أَنَّهُ قَالَ كَذَا وَكَذَا، فَرَجَعَ الْمَرَّةَ الْآخِرَةَ بِبِشَارَةٍ عَظِيمَةٍ، فَقَالَ: «اذْهَبْ إِلَيْهِ فَقُلْ لَهُ: إِنَّكَ لَسْتَ مِنْ أَهْلِ النَّارِ، وَلَكِنْ مِنْ أَهْلِ الْجَنَّةِ».

[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 3613]
المزيــد ...

Imepokewa kutoka kwa Anas bin Maalik -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-:
Yakwamba Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- siku moja alimkosa Thabiti bin Kaisi, mtu mmoja akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, mimi naweza kukupa taarifa zake, akamfuata akamkuta akiwa amekaa nyumbani kwake, akiwa ameinamisha kichwa chake, akasema: Ni jambo gani limekusibu? Akasema: Ni shari, alikuwa akinyanyua sauti yake juu ya sauti ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, tayari yameporomoka matendo yake, naye ni katika watu wa motoni, akarudi yule bwana kwa Mtume akamweleza kuwa kasema kadhaa wa kadhaa, mara ya pili akarudi kwake akiwa habari njema, akasema: "Nenda kwamwambie: Wewe si miongoni mwa watu wa motoni, bali ni katika watu wa peponi".

[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 3613]

Ufafanuzi

Alimkosa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- Thabiti bin Kaisi radhi za Allah ziwe juu yake, akamuulizia, mtu mmoja akasema: Mimi naweza kukupatia habari zake, na sababu ya kukosekana kwake, akamwendea akamkuta akiwa na huzuni na kainamisha kichwa chake nyumbani kwake, akamuuliza: Umepatwa na nini? Thabiti akamueleza shari aliyonayo; kwa sababu yeye alikuwa akinyanyua sauti yake juu ya sauti ya Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, na Mwenyezi Mungu kamuonya mwenye kufanya hivyo kwa kubatilika matendo yake, na kwamba yeye ni katika watu wa motoni.
Yule bwana akarejea kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- na akamueleza hilo, na Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akamuamrisha arudi kwa Thabiti na ampe habari njema, yakuwa yeye si miongoni mwa watu wa motoni bali ni katika watu wa peponi, na hii ni kwa sababu alikuwa ni mtu mwenye sauti ya juu kimaumbile, nakuwa yeye ndiye alikuwa mzungumzaji wa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- na ni mzungumzaji wa Answari (Watu wa Madina).

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Kituruki Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese Thai Pashto Kiassam Albanian السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية Luqadda qer-qeesiya النيبالية Luqadda yuruuba الليتوانية الدرية الصربية الصومالية Luqadda kiniya ruwadiga الرومانية المجرية التشيكية الموري Luqadda malgaashka الفولانية Kiitaliano Luqadda Oromaha Luqadda kinaadiga الولوف Luqadda Asariga الأوكرانية الجورجية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Kumebainishwa ubora wa Thabiti bin Kaisi radhi za Allah ziwe juu yake nakuwa ni katika watu wa peponi.
  2. Kuwajali Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- Masahaba na kuwafuatilia.
  3. Hofu ya Masahaba radhi za Allah ziwe juu yao ya kuogopa kuporomoka matendo yao.
  4. Uwajibu wa kuwa na adabu wakati wa kuzungumza na Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- enzi za uhai wake, na kupunguza sauti wakati wa kusikia mafundisho yake baada ya kifo chake.