+ -

عَنِ ‌ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا:
أَنَّ نَاسًا مِنْ أَهْلِ الشِّرْكِ، كَانُوا قَدْ قَتَلُوا وَأَكْثَرُوا، وَزَنَوْا وَأَكْثَرُوا، فَأَتَوْا مُحَمَّدًا صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَقَالُوا: إِنَّ الَّذِي تَقُولُ وَتَدْعُو إِلَيْهِ لَحَسَنٌ، لَوْ تُخْبِرُنَا أَنَّ لِمَا عَمِلْنَا كَفَّارَةً، فَنَزَلَ {وَالَّذِينَ لا يَدْعُونَ مَعَ اللهِ إِلَهًا آخَرَ وَلا يَقْتُلُونَ النَّفْسَ الَّتِي حَرَّمَ اللهُ إِلا بِالْحَقِّ وَلا يَزْنُونَ}[الفرقان: 68]، وَنَزَلَت: {قُلْ يَا عِبَادِيَ الَّذِينَ أَسْرَفُوا عَلَى أَنْفُسِهِمْ لا تَقْنَطُوا مِنْ رَحْمَةِ اللهِ} [الزمر: 53].

[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 4810]
المزيــد ...

Imepokewa kutoka kwa bin Abbas -Radhi za Allah ziwe juu yao yeye na baba yake-:
Yakwamba watu miongoni mwa washirikina walikuwa wameuwa watu, na wakakithirisha mauaji, na wakazini na wakikithirisha zinaa, wakamjia Muhammadi -Rehema na amani ziwe juu yake- wakasema: Hakika haya unayoyasema na kuwalingania watu ni mambo mazuri, ikiwa utatwambia juu ya haya tuliyoyafanya kama yana kafara, ikateremka kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Na wale ambao hawamuombi pamoja na Mwenyezi Mungu mungu mwingine na wala hawauwi nafsi aliyoiharamisha Mwenyezi Mungu isipokuwa kwa haki na wala hawazini" [Al-Furqan: 68], na ikateremka: "Sema: Enyi waja wangu waliojidhulumu nafsi zao! Msikate tamaa na rehema ya Mwenyezi Mungu..." [Az-Zumar: 53].

[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 4810]

Ufafanuzi

Walikuja watu miongoni mwa washirikina kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- na walikuwa wamekwisha fanya mauaji mengi na zinaa nyingi, wakasema kumwambia Mtume: Hakika Uislamu unaoulingania na mafundisho yake ni mazuri, lakini sisi tutakuwa na hali gani kwa yale tuliyoyatenda miongoni mwa ushirikina na madhambi makubwa, je, yanakafara?.
Zikateremka aya mbili, kiasi ambacho Mwenyezi Mungu aliwakubalia watu toba zao pamoja na wingi wa madhambi yao na ukubwa wake, na lau kama si hivyo basi wangeendelea kubaki katika ukafiri wao na ujeuri wao wala wasingeingia katika dini hii.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Kituruki Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese Thai Pashto Kiassam Albanian السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية Luqadda qer-qeesiya النيبالية Luqadda yuruuba الليتوانية الدرية الصربية الصومالية Luqadda kiniya ruwadiga الرومانية المجرية التشيكية الموري Luqadda malgaashka Kiitaliano Luqadda Oromaha Luqadda kinaadiga الولوف Luqadda Asariga الأوكرانية الجورجية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Ubora wa Uislamu na utukufu wake nakuwa Uislamu unabomoa madhambi yaliyokuwa kabla yake.
  2. Upana wa rehema ya Mwenyezi Mungu kwa waja wake na msamaha wake na kufuta kwake madhambi.
  3. Uharamu wa ushirikina, na uharamu wa kuua nafsi bila hatia, na uharamu wa zinaa, na ahadi ya adhabu kwa atakayeyasogelea ama kujiingiza katika madhambi haya.
  4. Toba ya kweli iliyoambatana na utakasifu (Ikhlaswi) na matendo mema, hufuta madhambi yote makubwa likiwemo la kumkufuru Mwenyezi Mungu Mtukufu.
  5. Uharamu wa kukata tamaa na kunyongeka katika rehema za Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka.