عَنِ ابْنِ مَسْعُودٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ، قَالَ: قَالَ رَجُلٌ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، أَنُؤَاخَذُ بِمَا عَمِلْنَا فِي الجَاهِلِيَّةِ؟ قَالَ: «مَنْ أَحْسَنَ فِي الإِسْلاَمِ لَمْ يُؤَاخَذْ بِمَا عَمِلَ فِي الجَاهِلِيَّةِ، وَمَنْ أَسَاءَ فِي الإِسْلاَمِ أُخِذَ بِالأَوَّلِ وَالآخِرِ».
[صحيح] - [متفق عليه]
المزيــد ...

Kutoka kwa bin Mas'udi Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, Amesema: Alisema mtu mmoja: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, Je tutaadhibiwa kwa yale tuliyoyafanya zama za ujinga? Akasema: "Atakayefanya mema katika uislamu hatoadhibiwa kwa yale aliyoyafanya zama za ujinga, na atakayefanya uovu katika uislamu ataadhibiwa kuanzia ya mwanzo mpaka ya mwisho".
Sahihi - Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim

Ufafanuzi

Mtu mmoja alimuuliza Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kuhusu yale waliyoyafanya zama za ujinga katika mabaya na maasi, je wataadhibiwa na watachukuliwa kwayo? Akasema Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-: Atakayefanya mema katika uislamu: Na wema katika uislamu ni kuendelea na dini yake na kuacha maasi- Hivyo hatohesabiwa kwa yale aliyoyafanya katika zama za ujinga miongoni mwa maasi, sawa sawa yawe ni katika madhambi makubwa kama kuua na kuzini, au madhambi madogo, na atakayefanya mabaya katika uislamu kama kuritadi (kutoka katika dini) basi atahesabiwa kwanzia yale aliyoyafanya katika ukafiri na yale aliyoyafanya katika uislamu, na kauli hii maana yake ni sahihi, ama ikisemekana kuwa ametenda mabaya maana yake ameasi na amefanya dhambi katika uislamu, basi dhahiri yake itakuwa inapingana na kile ambacho umma mzima wa kiislamu umekubaliana kuwa uislamu unafuta yaliyokuwa kabla yake, ambayo ni hadithi iko katika sahihi Muslim, Na amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Sema kuwaambia wale waliokufuru ikiwa kama watakoma yatasamehewa kwao yale yaliyopita, na ikiwa watarudia basi (tutawatesa kama) ilivyopita mifano ya watu wa zamani", na tafsiri nikuwa atamuumbua kwa yale aliyoyafanya katika ukafiri na atamkaripia, ni kana kwamba anaambiwa: Hivi kwani hukufanya kadhaa wa kadhaa na wewe ukiwa kafiri? Na ni kwanini usikuzuie uislamu wako kutokurudia tena mfano wa hayo pindi uliposilimu, kisha ataadhibiwa kwa madhambi aliyoyachuma, Yaani ndani ya uislamu, na yasemekana: Inawezekana ikawa maana ya kutenda mabaya ndani ya uislamu nikuwa asiwe na uislamu sahihi, na imani isiwe takasifu kwa kuwa kwake ni mnafiki na mfano wa hilo, na tasfiri ya kwanza ndio yenye kutegemewa zaidi.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibangali Kichina Kifursi Kihindi Kivetenamu Kisin-hala Ki ighori Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese Thai German Pashto Kiassam Albanian السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية الدرية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Kutilia umuhimu maswahaba Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao swala la matendo na kukubalika kwake.
  2. Kuhimizwa juu ya kufanya wema katika uislamu na kuacha maasi.
  3. Mwenye kuritadi kutoka katika uislamu atahesabiwa kwa matendo yake aliyoyafanya ndani ya uislamu na aliyoyafanya katika ukafiri.