عن أبي هريرة رضي الله عنه ، أن رسول الله صلى الله عليه وسلم قال: «الإيمانُ بِضْعٌ وَسَبْعُونَ أو بِضْعٌ وسِتُونَ شُعْبَةً: فَأَفْضَلُهَا قَوْلُ: لا إله إلا الله، وَأَدْنَاهَا إِمَاطَةُ الأَذَى عَنِ الطَّرِيقِ، وَالحَيَاءُ شُعْبَةٌ مِنَ الإِيمَانِ».
[صحيح] - [متفق عليه]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abuu Huraira Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, yakwamba Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake- Amesema: "Imani iko zaidi ya sehemu sabini au zaidi ya sehemu sitini: bora yake ni kauli ya: Laa ilaaha illa llaahu,- Hapana Mola ispokuwa Mwenyezi Mungu, na ya chini yake ni kuondoa udhia njiani, na aibu ni sehemu katika imani".
Sahihi - Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim

Ufafanuzi

Imani si jambo moja, au kigawanyo kimoja, lakini ni vigawanyo vingi, ni zaidi ya sabini, au ni zaidi ya sehemu sitini, lakini bora yake ni neno moja: nalo ni Laa ilaaha illa llaahu- Hapana Mola ispokuwa Mwenyezi Mungu, na nyepesi yake ni kuondoa kila kinachowaudhi wapitaji, kama jiwe, mwiba, au kinginecho, na aibu ni sehemu ya imani.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibangali Kichina Kifursi Kitagalogi Kihindi Kivetenamu Kisin-hala Kikurdi Kireno Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese Thai German Kijapani Pashto Kiassam Albanian
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Imani ina daraja baadhi yake zipo juu kuliko zingine.
  2. Imani kwa watu wa sunna ni kauli na vitendo na itikadi.
  3. Imani ni kichocheo na ni kigezo cha amali njema.
  4. Imani inagawanyika na ndio maana inaongezeka na kupungua.
  5. Imani ni jambo la kutafutwa.
  6. Ubora wa aibu na kuhimizwa kujipamba nayo.