عن أبي سعيد الخدري رضي الله عنه قال: سمعت رسول الله صلى الله عليه وآله وسلم يقول: «من رأى منكم منكراً فليُغيِّره بيده، فإلم يستطع فبلسانه، فإلم يستطع فبقلبه، وذلك أضعف الإيمان».
[صحيح] - [رواه مسلم]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abuu Saidi Al Khudriy Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake Amesema: Nilimsikia Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- Akisema: "Mwenye kuona miongoni mwenu jambo baya basi alibadilishe kwa mkono wake, ikiwa kama hatoweza basi kwa ulimi wake, ikiwa kama hatoweza basi kwa moyo wake, na huo ni udhaifu wa imani".
Sahihi - Imepokelewa na Imamu Muslim

Ufafanuzi

Amesema Abuu Saidi Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Nilimsikia Mtume Rehema na Amani ziwe juu yake akisema: Atakayeona miongoni mwenu jambo baya; na tamko hili linawahusu watu wote, linakusanya wanaume na wanawake, wadogo na wakubwa, na kila mmoja anaingia chini ya tamko la 'Yeyote, na miongoni mwenu' na Uovu ni kila jambo baya lenyewe, na hujulikana kwa mambo mawili: kukatazwa na sheria na akili kujulisha hivyo, lakini huwa halihusiani na kupata dhambi isipokuwa linapokuja kwa tamko la kisheria, na jambo jema ni kinyume cha hilo, na amri haiwi kwa mzaha tu na matamanio na matashi, kisha akabainisha Rehema na Amani ziwe juu yake ngazi za kuzuia uovu kulingana na jinsi inavyowezekana kwa muondoaji, akaanza na ngazi ya kwanza akasema: kwa mkono wake, na kuuondoa kwa mkono ni kwa yule mwenye mamlaka, au kwa mwenye kuweza ikiwa kwa njia ya hekima, na ikawa hakujaambatana kuzuia kwake na uovu mwingine au zaidi yake, ikiwa hatoweza kuuondoa kwa mkono basi kwa ulimi wake, na kwa ulimi inakuwa kwa utaratibu unaofaa kwa njia ambayo haina athari, na wala haiambatani na uovu mkubwa, ikiwa kama hatoweza kuuondoa kwa ulimi wake basi auondoe kwa moyo wake (kwa kuchukia), ikiwa kama atahofia madhara atakapozungumza kwa kuukemea basi aukemee moyoni mwake, na akereke na auchukie uovu huo, na inamlazimu pia kuondoka mahala palipo na uovu atakapoweza kufanya hivyo, na huo ni udhaifu wa imani, yaani, hii ni daraja ya chini mno ya alama hii ambayo ni miongoni mwa alama za imani; kwasababu hii inakuwa ni kiwango cha chini sana cha kuitekeleza.

Kufanya Tarjama: Lugha ya kiingereza Kiispania Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kirashia Kibaghali Kifursi Kihindi Kivetenamu Kisin-hala Kikurdi Kireno Kimalayo Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese Thai
Kuonyesha Tarjama

Faida nyingi

  1. Hadithi hii ni msingi katika ngazi za kuondoa uovu.
  2. Uwajibu wa kukemea uovu kwa kadiri ya uwezo.
  3. Kufanya sababu katika kuondoa uovu.
  4. Nikuwa mlango wa kuamrisha mema na kukataza maovu ni mlango mkubwa sana katika dini, ndio unaosimamia dini na kuimiliki.
  5. Sheria imezingatia tofauti ya uwezo wa watu katika kuondoa uovu.
  6. Kurudi katika Qur'ani na sunna kwa ajili ya kujua adhabu zinazoambatana na maovu, na si kwa kufuata matamanio.
  7. Kumuelekeza aliyechini ya mtu au aliyechini ya uangalizi wake, na kuondoa uovu utakapojitokeza kwao.
  8. Imani ina daraja, kauli na matendo na nia, nakuwa imani ina ngazi huzidi na kupungua.