+ -

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضيَ اللهُ عنهُ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:
«بَيْنَمَا رَجُلٌ يَمْشِي بِطَرِيقٍ وَجَدَ غُصْنَ شَوْكٍ عَلَى الطَّرِيقِ فَأَخَّرَهُ، فَشَكَرَ اللَّهُ لَهُ فَغَفَرَ لَهُ».

[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح مسلم: 1914]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema:
"Siku moja mtu mmoja alikuwa akipita njiani akakuta tawi la miba likiwa njiani akaliondosha, Allah akamshukuru na akamfutia madhambi yake".

[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح مسلم - 1914]

Ufafanuzi

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba siku moja kuna mtu mmoja alikuwa akitembea njiani akapita katika tawi mti wa miba likiwa barabarani likiwaudhi waislamu, akalivuta na akaliondosha njiani, basi Mwenyezi Mungu akamshukuru na akamsamehe.

Katika Faida za Hadithi

  1. Fadhila za kuondoa udhia njiani, na kwamba hilo ni sababu ya kuupata msamaha wa Mwenyezi Mungu.
  2. Kutodharau matendo mema hata yakiwa ni madogo.
  3. Uislamu ni dini ya usafi na kulinda mazingira na amani ya jamii nzima.
Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kiassam الهولندية الغوجاراتية الرومانية المجرية الجورجية
Kuonyesha Tarjama