عن جابر بن عبد الله رضي الله عنهما عن النبي صلى الله عليه وسلم قال:
«كُلُّ مَعْرُوفٍ صَدَقَةٌ».

[صحيح] - [رواه البخاري من حديث جابر، ورواه مسلم من حديث حذيفة] - [صحيح البخاري: 6021]
المزيــد ...

Imepokelewa kutoka kwa Jaabir -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- kuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema:
"Kila wema ni sadaka"

[Sahihi] - [Imepokelewa na Bukhari kutokana na hadithi ya Jaabir, na amepokea Muslim kutokana na hadithi ya Hudhaifa] - [Swahiih Al Bukhaariy - 6021]

Ufafanuzi

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa kila wema na kuwanufaisha wengine kuanzia kauli au matendo huwa ni sadaka, na kuna malipo na thawabu.

Katika Faida za Hadithi

  1. Nikuwa sadaka haishii tu katika vile anavyovitoa mtu katika mali yake, bali inajumuisha kila kheri anayoifanya mwanadamu au kuitamka na kuifikisha kwa wengine.
  2. Hapa kuna himizo la kutenda wema, na kila jambo lenye manufaa kwa wengine.
  3. Kutodharau kitu katika wema, hata kama ni kidogo.
Kuonyesha Tarjama
Lugha: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Ziada (67)