عن أنس بن مالك رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : «كلُّ بني آدم خَطَّاءٌ، وخيرُ الخَطَّائِينَ التوابون».
[حسن] - [رواه الترمذي وابن ماجه والدارمي وأحمد]
المزيــد ...
Kutoka kwa Anas bin Malik- Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Allah- Rehma na amani ziwe juu yake- "Kila mwanadamu ni mkosefu, na mbora wa wakosefu ni wale wenye kutubia".
[Ni nzuri] - [Imepokelewa na Ibnu Maajah - Imepokelewa na Imamu Tirmidhiy - Imepokelewa na Ahmad - Imepokelewa na Addaaramy]
Haepukani mwanadamu na kukosea, kwa jinsi alivyoumbwa kutokana na udhaifu, na kutokumtii msimamizi wake katika kutekeleza yale aliyomtaka ayafanye, na kuacha yale aliyomkataza, lakini yeye Mtukufu amefungua mlango wa toba kwa waja wake, na akaeleza kuwa mbora wa wakosefu ni wale wenye kukithirisha toba.