عن أبي مسعود البدري رضي الله عنه مرفوعاً: «إذا أَنْفَقَ الرجلُ على أهله نَفَقَةً يَحْتَسِبُهَا فهي له صَدَقَةٌ».
[صحيح] - [متفق عليه]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abii Mas'udi Al-Badriy- Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Hadithi Marfu'u: "Atakapotoa mtu kwa familia yake tumizi lolote akitaraji malipo basi hilo kwake ni sadaka".
Sahihi - Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim
Atakapotoa mtu kwa watu wake ambao inamlazimu kuwahudumia kama mke wake na mtoto wake, na wengineo hivyo hivyo, naye akikusudia kujikaribisha kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa hilo na akitaraji malipo kwa kile anachokitoa, basi yeye analipwa kwa tumizi hilo kama malipo ya sadaka kwa mafakiri na mfano wao katika njia za wema.