عَنْ عَائِشَةَ أُمِّ المؤْمنينَ رَضيَ اللهُ عنها قَالَت:
دَخَلَتْ هِنْدٌ بِنْتُ عُتْبَةَ امْرَأَةُ أَبِي سُفْيَانَ عَلَى رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَقَالَتْ: يَا رَسُولَ اللهِ، إِنَّ أَبَا سُفْيَانَ رَجُلٌ شَحِيحٌ، لَا يُعْطِينِي مِنَ النَّفَقَةِ مَا يَكْفِينِي وَيَكْفِي بَنِيَّ إِلَّا مَا أَخَذْتُ مِنْ مَالِهِ بِغَيْرِ عِلْمِهِ، فَهَلْ عَلَيَّ فِي ذَلِكَ مِنْ جُنَاحٍ؟ فَقَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «خُذِي مِنْ مَالِهِ بِالْمَعْرُوفِ مَا يَكْفِيكِ وَيَكْفِي بَنِيكِ».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح مسلم: 1714]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake amesema:
Aliingia Hindu binti Utba mke wa Abuu Sufiani kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hakika Abuu Sufiani ni mwanaume bahili sana, hanipi matumizi yanayonitosha mimi na wanangu isipokuwa kiasi ninachokichukua katika mali yake pasina yeye kujua, je kwa hilo nina tatizo? Akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Chukua katika mali yake kwa wema, kiasi kinachokutosha wewe na wanao".
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح مسلم - 1714]
Alitaka kujua Hindu binti Utba radhi za Allah ziwe juu yake kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu mume wake Abuu Sufiani radhi za Allah ziwe juu yake, na kwamba yeye ni mwanaume bahili mwenye pupa sana na mali yake, hampi katika matumizi kiasi kinachomtosha yeye na wanaye, mpaka achukue katika mali yake kwa siri hali yakuwa hajui, je ana dhambi juu yake katika hilo?. Akasema rehema na amani ziwe juu yake: Chukua kwa ajili yako na watoto wako katika mali yake kiasi kinachojulikana katika mazingira ya kawaida na kwamba hicho ndicho kitakachomtosheleza hata asipojua.