عَنْ عَائِشَةَ أُمِّ المؤْمنينَ رَضيَ اللهُ عنها قَالَت: قَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«تُقْطَعُ اليَدُ فِي رُبُعِ دِينَارٍ فَصَاعِدًا».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 6789]
المزيــد ...
Kutoka kwa Aisha -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-:
"Mkono unakatwa kwa robo Dinari na kuendelea".
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 6789]
Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa mwizi unakatwa mkono wake kwa kuiba robo Dinari ya dhahabu, na zaidi ya hapo, na kiwango chake kinalingana na kiasi cha Gramu 1.06 ya dhahabu.