عن عبد الله بن مَسعود رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم : «أَوَّلُ مَا يُقْضَى بَيْنَ النَّاسِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ فِي الدِّمَاءِ».
[صحيح] - [متفق عليه، واللفظ لمسلم]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abdallah bin Mas'udi -Radhi za Mwenyezi Mungu- Amesema: Amesema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake- : "La kwanza litakalohukumiwa kati ya watu siku ya kiyama ni katika damu".
Sahihi - Imepokelewa na Al-Bukhaariy na Muslim na tamko ni la Muslim

Ufafanuzi

Atawahesabu Mwenyezi Mungu -Mtukufu- viumbe siku ya kiyama, kisha atawahukumu baina yao kwa uadilifu, na ataanza na dhulma kwa umuhimu wake, na kwasababu yakuwa damu ndio kubwa na muhimu zaidi katika vile vinavyofanyika katika dhulma, kwani yenyewe ndiyo ya kwanza kuhukumiwa katika siku hiyo tukufu, na hii ni kati ya waja katika dhulma, ama matendo ya mja la kwanza kutazamwa ni swala.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibangali Kichina Kifursi Kitagalogi Kihindi Kivetenamu Kisin-hala Ki ighori Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Thai Pashto Kiassam السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية الدرية
Kuonyesha Tarjama