+ -

عَنْ أَبِي مُوسَى الأَشْعَرِيِّ رضي الله عنه قَالَ:
أَتَيْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي رَهْطٍ مِنَ الأَشْعَرِيِّينَ أَسْتَحْمِلُهُ، فَقَالَ: «وَاللَّهِ لاَ أَحْمِلُكُمْ، مَا عِنْدِي مَا أَحْمِلُكُمْ» ثُمَّ لَبِثْنَا مَا شَاءَ اللَّهُ فَأُتِيَ بِإِبِلٍ، فَأَمَرَ لَنَا بِثَلاَثَةِ ذَوْدٍ، فَلَمَّا انْطَلَقْنَا قَالَ بَعْضُنَا لِبَعْضٍ: لاَ يُبَارِكُ اللَّهُ لَنَا، أَتَيْنَا رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ نَسْتَحْمِلُهُ فَحَلَفَ أَنْ لاَ يَحْمِلَنَا فَحَمَلَنَا، فَقَالَ أَبُو مُوسَى: فَأَتَيْنَا النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَذَكَرْنَا ذَلِكَ لَهُ، فَقَالَ: «مَا أَنَا حَمَلْتُكُمْ، بَلِ اللَّهُ حَمَلَكُمْ، إِنِّي وَاللَّهِ -إِنْ شَاءَ اللَّهُ- لا أَحْلِفُ عَلَى يَمِينٍ، فَأَرَى غَيْرَهَا خَيْرًا مِنْهَا، إِلَّا كَفَّرْتُ عَنْ يَمِينِي، وَأَتَيْتُ الَّذِي هُوَ خَيْرٌ».

[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 6718]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abuu Musa Al-Ash'ary radhi za Allah ziwe juu yake amesema:
Nilikuja kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake nikiwa na kundi la Ash’ari ili kumuomba atuchukue, akasema: “Wallahi sitokuwa na chochote cha kukubebeni ” Kisha tukakaa muda kidogo aliopenda Mwenyezi Mungu tukae, tukaletewa ngamia, akaamrisha tupewe wanyama watatu kwa ajili yetu, tulipoondoka wakasema baadhi yetu kuwaambia wengine: Mwenyezi Mungu hatotubariki, tumemuendea Mtume rehema na amani ziwe juu yake tukamuomba atubebe katika vipando lakini akaapa kuwa hatotubeba, kisha akatubeba, akasema Abuu Musa: Basi tukaja kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake tukamueleza hilo, akasema: “Si mimi niliyekubebeni, bali Mwenyezi Mungu ndiye aliyekubebeni Wallahi – akipenda Mwenyezi Mungu - sitokula kiapo cha jambo fulani isipokuwa ninapoona kilichobora zaidi basi huwa ninatoa kafara ya kiapo changu kisha ninafanya lililo bora zaidi.”

[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 6718]

Ufafanuzi

Anasimulia Abuu Musa Al-Ash’ari radhi za Allah ziwe juu yake kuwa, alikuja kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake akiwa na kundi la kabila lake, na makusudio yao yalikuwa kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, ili awape ngamia wapande, ili kuweza kushiriki katika jihadi, aliapa rehema na amani ziwe juu yake kuwa hatowabeba, na hakuwa hana chochote cha kuwabeba, basi wakarudi na kukaa kwa muda, kisha wakaletewa ngamia watatu kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akawatumia wale mabwana, baadhi yao wakaambiana: Mwenyezi Mungu asitubariki kwa ngamia hawa; Kwa sababu Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliapa kutotubeba, basi wakamjia na wakamuuliza, akasema rehema na amani ziwe juu yake: Aliyekubebeni ni Mwenyezi Mungu Mtukufu; Kwa sababu yeye ndiye aliyetoa ufanikishaji na akaruzuku, lakini mimi ni sababu ya haya kutokea kupitia mikono yangu, kisha akasema rehema na amani ziwe juu yake: Wallahi, akipenda Mwenyezi Mungu, sitaapa kufanya au kuacha chochote, na nikaona kuwa kisichokuwa kiapo hicho ni heri na bora zaidi, isipokuwa nitafanya lililo bora zaidi, na kuyaacha niliyoapa, na ninalipa kafara ya kiapo changu.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Thai Pashto Kiassam السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية Luqadda qer-qeesiya النيبالية الليتوانية الدرية الصربية الرومانية الموري Luqadda malgaashka Luqadda Oromaha Luqadda kinaadiga الجورجية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Inafaa kuapa bila kutakwa kuapa; ili kuitia mkazo habari hata kama ni ya jambo la baadae.
  2. Inajuzu kutojipa uhakika kwa kusema “Mwenyezi Mungu akipenda” baada ya kiapo, ikiwa kutafanywa kwa nia na kiapo na kukaunganishwa nacho, basi kafara haitohitajika kwa mwenye kuvunja kiapo chake.
  3. Himizo la kuvunja kiapo ikiwa ataona jambo bora kuliko hilo, na atatoa kafara ya kiapo chake.