عَنِ ابْنِ عُمَرَ رضي الله عنهما:
عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَنَّهُ نَهَى عَنِ النَّذْرِ، وَقَالَ: «إِنَّهُ لَا يَأْتِي بِخَيْرٍ، وَإِنَّمَا يُسْتَخْرَجُ بِهِ مِنَ الْبَخِيلِ».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح مسلم: 1639]
المزيــد ...
Kutoka kwa bin Omari -Radhi za Allah ziwe juu yao yeye na baba yake-:
Kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- Amekataza kuweka nadhiri, na akasema: "Hakika nadhiri haiji kwa kheri, bali hutolewa kwayo (vilivyo) kwa bahili"
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح مسلم - 1639]
Amekataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuweka nadhiri, nayo ni mtu kujiwajibishia kitu ambacho sheria haijamlazimisha kukifanya, na akasema kuwa: Nadhiri haiwahishi kitu na wala haikicheleweshi, bali hutolewa vilivyo kwa mtu bahili ambaye hafanyi ila yale ya wajibu pekee, nakuwa nadhiri haileti kitu ambacho hakikukadiriwa.