عَنْ عَلِيٍّ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:
«مَنْ أَصَابَ حَدًّا فَعُجِّلَ عُقُوبَتَهُ فِي الدُّنْيَا فَاللَّهُ أَعْدَلُ مِنْ أَنْ يُثَنِّيَ عَلَى عَبْدِهِ العُقُوبَةَ فِي الآخِرَةِ، وَمَنْ أَصَابَ حَدًّا فَسَتَرَهُ اللَّهُ عَلَيْهِ وَعَفَا عَنْهُ فَاللَّهُ أَكْرَمُ مِنْ أَنْ يَعُودَ فِي شَيْءٍ قَدْ عَفَا عَنْهُ».
[حسن] - [رواه الترمذي وابن ماجه] - [سنن الترمذي: 2626]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Ally -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema:
"Atakayefanya jambo la kustahiki kuadhibiwa, ikaharakishwa adhabu yake basi Mwenyezi Mungu ni muadilifu zaidi juu ya mja wake (hawezi) kumuadhibu mara mbili akhera, na atakayefanya jambo la kustahiki kuadhibiwa, Mwenyezi Mungu akamsitiri na akamsamehe, basi Mwenyezi Mungu ni mkarimu zaidi (hawezi) kurudi katika jambo ambalo alikwishalisamehe".
[Ni nzuri] - - [سنن الترمذي - 2626]
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa yeyote atakayefanya dhambi zinazohitaji adhabu ya kisheria, kama vile uzinzi au wizi, na akapata adhabu hiyo na ikatekelezwa duniani, basi adhabu hiyo itamfutia dhambi hiyo na kumuondolea adhabu ya Akhera. Hii ni kwa sababu Allah ni mkarimu na mwenye rehema, na hawezi kumuhukumu mja wake kwa adhabu moja mara mbili. Na ikiwa Allah amemsitiri mja wake duniani na hakumuhukumu kwa dhambi hiyo, na akamsamehe na kumghufiria, basi Allah Mtukufu ni mkarimu na mbora zaidi hawezi kurudi katika adhabu ya dhambi aliyoisamehe na kuifuta."