+ -

عَنْ عُبَادَةَ بْنِ الصَّامِتِ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ، وَكَانَ شَهِدَ بَدْرًا، وَهُوَ أَحَدُ النُّقَبَاءِ لَيْلَةَ العَقَبَةِ: أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ، وَحَوْلَهُ عِصَابَةٌ مِنْ أَصْحَابِهِ:
«بَايِعُونِي عَلَى أَلَّا تُشْرِكُوا بِاللَّهِ شَيْئًا، وَلاَ تَسْرِقُوا، وَلاَ تَزْنُوا، وَلاَ تَقْتُلُوا أَوْلاَدَكُمْ، وَلاَ تَأْتُوا بِبُهْتَانٍ تَفْتَرُونَهُ بَيْنَ أَيْدِيكُمْ وَأَرْجُلِكُمْ، وَلاَ تَعْصُوا فِي مَعْرُوفٍ، فَمَنْ وَفَى مِنْكُمْ فَأَجْرُهُ عَلَى اللَّهِ، وَمَنْ أَصَابَ مِنْ ذَلِكَ شَيْئًا فَعُوقِبَ فِي الدُّنْيَا فَهُوَ كَفَّارَةٌ لَهُ، وَمَنْ أَصَابَ مِنْ ذَلِكَ شَيْئًا ثُمَّ سَتَرَهُ اللَّهُ فَهُوَ إِلَى اللَّهِ، إِنْ شَاءَ عَفَا عَنْهُ وَإِنْ شَاءَ عَاقَبَهُ» فَبَايَعْنَاهُ عَلَى ذَلِكَ.

[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 18]
المزيــد ...

Kutoka kwa Ubada bin Swamiti radhi za Allah ziwe juu yake, na alikuwa miongoni mwa walioshuhudia vita vya Badri, naye alikuwa ni mmoja wa vigogo katika usiku wa Aqaba: Ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alisema na pembezoni mwake kukiwa na jopo la Maswahaba zake:
"Nipeni ahadi ya utiifu ya kuwa msimshirikishe Mwenyezi Mungu na kitu chochote, na wala msiibe, na wala msizini, na wala msiwauwe watoto wenu, na wala msilete uzushi mtakouzua kwa mikono yenu na miguu yenu, na wala msiasi katika wema, basi atakayeyatimiza hayo miongoni mwenu basi malipo yake yatakuwa juu ya Mwenyezi Mungu, na atakayetenda lolote katika hayo akaadhibiwa katika dunia basi hiyo ndiyo kafara kwake, na atakayetenda lolote katika hayo kisha Mwenyezi Mungu akamsitiri basi hilo litabakia kwa Mwenyezi Mungu akitaka atamsamehe na akitaka atamuadhibu" Tukampa ahadi ya utiifu juu ya hayo.

[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 18]

Ufafanuzi

Ameeleza Ubada bin Swamiti radhi za Allah ziwe juu yake, na alikuwa ni miongoni mwa walioshuhudia vita vya Bardi kuu, naye akiwa kiongozi wa watu wake waliokuja kutoa mkono wa ahadi ya uaminifu kwa ajili ya kumnusuru Mtume rehema na amani ziwe juu yake usiku wa Aqaba ambayo iko Mina, wakati Mtume akiwa Makka kabla ya kuhama kwake kwenda Madina, ni kuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa kakaa na Maswahaba zake akawataka wamuahidi juu ya mambo haya: La kwanza: Wasishirikishe katika ibada za Mwenyezi Mungu kitu chochote hata kikiwa kidogo. La pili: Wasiibe. La tatu: Wasifanye uchafu wa zinaa. La nne: Wasiwauwe watoto wao; wa kiume kwa kuhofia ufakiri na umasikini au watoto wa kike kwa kuhofia fedheha. La tano: Wasilete uongo wataoutengeneza baina ya mikono yao na miguu yao, kwa sababu matendo mengi hutokea kupitia hivi viwili hata kama viungo vingine vitashiriki. La sita: Wasimuasi Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika jambo jema. Atakayethubutu miongoni mwao katika ahadi na akashikamana nayo basi malipo yake yako kwa Mwenyezi Mungu, na atakayefanya lolote miongoni mwa hayo yaliyotajwa -kasoro ushirikina- akaadhibiwa katika dunia kwa kusimamishiwa adhabu juu yake basi hilo ndio kafara yake, na kwa hilo dhambi lake litaondoka, na atakayefanya lolote miongoni mwa hayo kisha Mwenyezi Mungu akamsitiri basi huyu jambo lake liko kwa Mwenyezi Mungu; akitaka atamsamehe na akitaka atamuadhibu, wote waliokuwepo wakampa ahadi ya utiifu juu ya hayo.

Tafsiri: Lugha ya Kiindonesia Kivetenamu Kihausa Kiassam الأمهرية الهولندية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Kumebainishwa mambo yaliyoambatana na ahadi ya Aqaba ya kwanza huko Makka kabla hawajafaradhishiwa Jihadi.
  2. Amesema As-Sanadi: Kauli yake: "Katika wema": Haifichikani kuwa amri zake zote ni wema na haifikiriki kuwa na kinyume chake, kauli yake: "katika wema" hii ilikuwa ni kwa ajili ya kutanabahisha sababu ya kutii na kwamba hakuna kumtii kiumbe katika jambo lisilokuwa jema, na kwamba ni sharti katika utii kuwe na wema katika ahadi, na si utii wa moja kwa moja.
  3. Amesema Muhammadi bin Suleiman Attaimi na wengineo: Ametaja swala la mauaji ya watoto pekee; kwa sababu ni mauaji na ni kukata ukoo, hivyo kutilia umuhimu katazo hilo kunakuwa na mkazo zaidi, na ni kwa sababu hilo lilikuwa limezagaa sana kwao, jambalo ni kuwazika watoto wa kike na kuwauwa watoto wa kiume kwa kuhofia umasikini, au kawataja maalumu; ili wasijitetee kwa hilo.
  4. Amesema Nawawi: Ujumla wa hadithi hii umeondolewa kwa kauli yake Mtukufu: "Hakika Mwenyezi Mungu hasamehi kushirikishwa", Mwenye kuritadi anapouawa kwa sababu ya kutoka katika dini kuuawa hakuwi kafara kwake.
  5. Amesema Al-Kadhi Iyadhi: Wamesema wanachuoni wengi kuwa adhabu za kisheria ni kafara.