+ -

عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ:
قَدِمَ أُنَاسٌ مِنْ عُكْلٍ أَوْ عُرَيْنَةَ، فَاجْتَوَوْا المَدِينَةَ فَأَمَرَهُمُ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِلِقَاحٍ، وَأَنْ يَشْرَبُوا مِنْ أَبْوَالِهَا وَأَلْبَانِهَا، فَانْطَلَقُوا، فَلَمَّا صَحُّوا قَتَلُوا رَاعِيَ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، وَاسْتَاقُوا النَّعَمَ، فَجَاءَ الخَبَرُ فِي أَوَّلِ النَّهَارِ، فَبَعَثَ فِي آثَارِهِمْ، فَلَمَّا ارْتَفَعَ النَّهَارُ جِيءَ بِهِمْ، فَأَمَرَ فَقَطَعَ أَيْدِيَهُمْ وَأَرْجُلَهُمْ، وَسُمِرَتْ أَعْيُنُهُمْ، وَأُلْقُوا فِي الحَرَّةِ، يَسْتَسْقُونَ فَلاَ يُسْقَوْنَ، قَالَ أَبُو قِلاَبَةَ: فَهَؤُلاَءِ سَرَقُوا وَقَتَلُوا، وَكَفَرُوا بَعْدَ إِيمَانِهِمْ، وَحَارَبُوا اللَّهَ وَرَسُولَهُ.

[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 233]
المزيــد ...

Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maalik -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema:
Walikuja watu kutoka kabila la Ukli au Uraina, wakauchukia mjini Madina, kwa sababu hali ya hewa ya Madina haikuwafaa. Mtume rehema na amani ziwe juu yake akawaamuru waende katika ngamia wa zaka na wanywe mikojo yake na maziwa yake. Wakaondoka, na baada ya afya yao kurejea, wakamuua mchungaji wa ngamia wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na wakaiba ngamia hao. Habari zikamfikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake mapema asubuhi, basi akatuma watu kuwafuatilia, na wakapatikana kabla ya mchana. Mtume rehema na amani ziwe juu yake akaamuru mikono na miguu yao ikatwe, macho yao yakachomwa moto, na wakatupwa kwenye jangwa la mawe (Al-Harra). Wakawa wakiomba maji, lakini hawakupewa. Abu Qilaba anasema: Watu hawa walifanya wizi, wakafanya mauaji, walitoka katika Uislamu baada ya kuwa Waislamu, na walitangaza vita dhidi ya Mwenyezi Mungu na Mtume Wake.

[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 233]

Ufafanuzi

Walikuja watu kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, kutoka katika kabila la Ukli na Uraina wakiwa ni Waislamu, wakapatwa na ugonjwa na maradhi mazito kwao, yakavimba matumbo yao, wakachukia kuishi Madina kwa sababu chakula hakikuwapendeza wala hali ya hewa. Mtume rehema na amani ziwe juu yake akawaamuru waende katika ngamia za sadaka, na wanywe mikojo na maziwa yake. Wakaenda, na walipopona, na wakanenepa, na rangi zao zikarejea kuwa nzuri, wakamuua mchungaji wa ngamia wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na wakachukua ngamia. Habari hiyo ilifika asubuhi na mapema, ndipo Mtume akatuma kikosi cha kuwafuata. Wakawakamata, wakati wa jua kupanda juu wakaletwa wakiwa mateka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake. Mtume akaamuru mikono yao na miguu yao ikatwe, na macho yao yakatobolewa, kwa sababu walimtendea hivyo mchungaji. Kisha wakatupwa kwenye eneo lenye joto (al-Harra), wakawa wakiwaomba maji lakini hawakupewa mpaka walipokufa. Amesema Abuu Qilaba: Ni kwamba wao waliiba, na wakaua, na wakakufuru baada ya imani yao, na wakampiga vita Mwenyezi Mungu na Mtume wake.

Katika Faida za Hadithi

  1. Usafi wa mkojo wa kila kinacholiwa nyama yake.
  2. Sheria ya kujitibu kwa maziwa ya ngamia na mikojo yake.
  3. Sheria ya kufananisha katika kisasi, na katazo la kusulubu litachukuliwa pale panapokuwa hakuna mfanano na kisasi.
  4. Kuua kundi la watu kwa sababu ya mtu mmoja ni sawa, iwe walimuuwa kwa hila au kwa wizi wa kutumia silaha.
Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiindonesia Kisin-hala Kivetenamu Kihausa Kiassam الهولندية الغوجاراتية الرومانية المجرية الجورجية
Kuonyesha Tarjama