عن أبي موسى الأشعري رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه وسلم قال: «مَنْ حَمَلَ عَلَيْنَا السِّلاحَ فَلَيْسَ مِنَّا».
[صحيح] - [متفق عليه]
المزيــد ...

Na kutoka kwa Abii Musa Al-Ash'ariy radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, kutoka kwa Mtume rehema na Amani zimfikie, amesema: "Atakayetubebea silaha, si miongoni mwetu".
Sahihi - Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim

Ufafanuzi

Amebainisha Nabii rehema na Amani ziwe juu yake kuwa waumini wote ni ndugu, wanaumia baadhi yao kwa maumivu ya wengine, na ana furahi kwa furaha yake, na kuwa kauli yao ni moja, hivyo wao ni wamoja dhidi ya yule mwenye kuwafanyia uadui.basi inawalazimu kuwa pamoja na utiifu kwa kiongozi wao, na kumsaidia juu ya yule mwenye kumfanyia ujeuri na akatoka katika utiifu wake; kwasababu huyu mwenye kujitoa kapasua umoja wa waislamu, na kawabebea silaha, na akawaogopesha ikalazimu kupigana naye, mpaka arejee na atii amri ya Mwenyezi Mungu Mtukufu; kwasababu mwenye kujitoa kwao na akawafanyia uadui, hana mapenzi ya uislamu katika moyo wake, na katika hadithi hii kuna ahadi kali ya adhabu inayoonyesha kuwa maasi haya ni katika madhambi makubwa, yanayo maanisha ahadi kali na kemeo, hivyo ikalazimu kupigana naye na kumtia adabu.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibangali Kichina Kifursi Kitagalogi Kihindi Kivetenamu Kisin-hala Ki ighori Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese Thai German Kijapani Pashto Kiassam Albanian السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية الدرية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Kuharamishwa kujitoa kwa viongozi, nao ni mahakimu (watawala), hata kama yatajitokeza kwao baadhi ya maovu, madam hayajafikia katika ukafiri, kwasababu yanayoambatana na kujitoa kwao ni kupoteza roho, na kuwauwa wasio na hatia, na kuwaogopesha waislamu na Amani kutoweka, na kuvuruga utaratibu, hayo ni madhara makubwa kuliko kubakia kwao.
  2. Ikiwa kujitoa kumeharamishwa katika upande wa watawala ambao wanafanya baadhi ya maovu, Je kwa hali ya walionyooka na ni waadilifu?
  3. Uharamu wa kuwahofisha waislamu kwa silaha na kinginecho, hata kama ni kwa mzaha.