+ -

عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ قَالَ: خَرَجَ مُعَاوِيَةُ عَلَى حَلْقَةٍ فِي الْمَسْجِدِ، فَقَالَ: مَا أَجْلَسَكُمْ؟ قَالُوا: جَلَسْنَا نَذْكُرُ اللهَ، قَالَ آللَّهِ مَا أَجْلَسَكُمْ إِلَّا ذَاكَ؟ قَالُوا: وَاللهِ مَا أَجْلَسَنَا إِلَّا ذَاكَ، قَالَ: أَمَا إِنِّي لَمْ أَسْتَحْلِفْكُمْ تُهْمَةً لَكُمْ، وَمَا كَانَ أَحَدٌ بِمَنْزِلَتِي مِنْ رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أَقَلَّ عَنْهُ حَدِيثًا مِنِّي:
وَإِنَّ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ خَرَجَ عَلَى حَلْقَةٍ مِنْ أَصْحَابِهِ، فَقَالَ: «مَا أَجْلَسَكُمْ؟» قَالُوا: جَلَسْنَا نَذْكُرُ اللهَ وَنَحْمَدُهُ عَلَى مَا هَدَانَا لِلْإِسْلَامِ، وَمَنَّ بِهِ عَلَيْنَا، قَالَ: «آللَّهِ مَا أَجْلَسَكُمْ إِلَّا ذَاكَ؟» قَالُوا: وَاللهِ مَا أَجْلَسَنَا إِلَّا ذَاكَ، قَالَ: «أَمَا إِنِّي لَمْ أَسْتَحْلِفْكُمْ تُهْمَةً لَكُمْ، وَلَكِنَّهُ أَتَانِي جِبْرِيلُ فَأَخْبَرَنِي أَنَّ اللهَ عَزَّ وَجَلَّ يُبَاهِي بِكُمُ الْمَلَائِكَةَ».

[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 2701]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abuu Said Al-Khudri amesema: Muawia alitoka kwenda msikitini akakuta kundi, akasema: Nini kimewakalisha hapa? Wakasema: Tumekaa tukimkumbuka Mwenyezi Mungu. Akasema: Mnamuapa Mwenyezi Mungu kuwa hakuna lililowakalisha isipokuwa hilo? Wakasema: Wallahi hakuna lililotukalisha isipokuwa hilo. Akasema: Basi tambueni kuwa sikukuapisheni kwa sababu ya kuwatuhumu kwa lolote, na hakuna aliyekuwa katika nafasi yangu kwakuwa na mazungumzo machache zaidi kuliko mimi kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake:
Na hakika Mjumbe wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake, siku moja alitoka kwenda katika kundi la Maswahaba zake na kusema: “Mbona mmekaa pamoja?” Wakasema: Tumekaa tukimkumbuka Mwenyezi Mungu na kumhimidi kwa kuwa ametuongoza kwenye Uislamu, na kwa kutujaalia. Akasema: “Mnamuapa Mwenyezi Mungu kuwa hakuna lililokukalisheni isipokuwa hilo?" Wakasema: "Wallahi hatukukaa kwa lolote ila hilo.” Akasema: «Ama mimi sikukuapisheni kwa sababu ya kuwatuhumu, lakini Jibril alinijia na kuniambia kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu anajifaharisha kupitia nyinyi, huko kwa Malaika.!"

[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 2701]

Ufafanuzi

Alitoka Muawia bin Abi Sufian, Mwenyezi Mungu awawie radhi, kwenda katika kundi moja msikitini na akawauliza wamekusanyika kwa jambo gani, Wakasema: Tunamtaja Mwenyezi Mungu, basi akawaapisha, Mwenyezi Mungu awe radhi naye, kwamba hawakutaka katika kikao chao na mkusanyiko wao isipokuwa ni kumtaja Mwenyezi Mungu, wakaapa kwa hilo, kisha akawaambia: Sikukuapisheni kwa tuhuma yoyote juu yenu au kuwa na shaka juu ya ukweli wenu, kisha akaeleza kuhusu hali yake kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na kwamba hakuna aliyekuwa karibu naye kuliko yeye. Kwa sababu Ummu Habiba alikuwa ni dada yake, mke wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na kwa sababu alikuwa ni miongoni mwa waandishi wa wahyi, lakini ilikuwa ni nadra sana kusimulia hadithi, Basi akawaambia kuwa Mtume, rehema na amani ziwe juu yake, siku moja alitoka nyumbani kwake na akawakuta wamekaa msikitini wakimdhukuru Mwenyezi Mungu na kumhimidi kwa yale aliyowaongoza katika Uislamu na kuwakirimia. Mwenyezi Mungu amfikishie rehema na amani, akawauliza na kuwaapisha sawa na alivyofanya Muawia kwa jamaa zake, Mwenyezi Mungu amuwie radhi. Kisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake akawaambia kuhusu sababu ya kuwauliza kwake na kuapa kwao: kwamba Malaika Jibril, amani iwe juu yake, alimjia na kumwambia kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu anajifakhirisha kupitia nyinyi kwa Malaika, na anawadhihirishia ubora wenu na anawaonyesha uzuri wa amali yenu, na anakusifieni mbele yao.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Thai Pashto Kiassam السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية Luqadda qer-qeesiya النيبالية Luqadda yuruuba الليتوانية الدرية الصربية الصومالية Luqadda kiniya ruwadiga الرومانية الموري Luqadda malgaashka Luqadda Oromaha Luqadda kinaadiga الجورجية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Fadhila za Muawia, Mungu amuwie radhi, na pupa yake ya kumuiga Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake katika kufikisha elimu.
  2. Inafaa kumwapiza mtu hata kama humtuhumu, bali kwa ajili tu kumzindua juu ya umuhimu wa kheri unayotaka kumueleza.
  3. Fadhila za vikao vya kumtaja Mwenyezi Mungu, na vikao vya kielimu, nakuwa Mwenyezi Mungu huvipenda na hujifaharisha kwavyo mbele za Malaika.