عن عبد الله بن عباس رضي الله عنهما قال: مر النبي صلى الله عليه وسلم بقبرين، فقال: «إنهما ليُعذَّبان، وما يُعذَّبان في كبير؛ أما أحدهما: فكان لا يستتر من البول، وأما الآخر: فكان يمشي بالنميمة».
[صحيح] - [متفق عليه]
المزيــد ...

Kutoka kwa Abdillahi bin Omar -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- Amesema: "Alipita Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- katika makaburi mawili, Akasema: Hakika hawa wawili wanaadhibiwa, na hawadhibiwi kwa madhambi makubwa; ama mmoja wao: alikuwa hajisitiri kutokana na mkojo, na ama huyu mwingine: Alikuwa akitembea akiwafitinisha watu".
Sahihi - Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim

Ufafanuzi

Alipita Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- wakiwa pamoja naye baadhi ya maswahaba wake katika makaburi mawili, akamfunulia Mwenyezi Mungu Mtukufu kwake kuhusu hali zao, nakuwa wao wanaadhibiwa, akawaeleza maswahaba zake kwa hilo, kwa kuutahadharisha umma wake na kwa kuuhofisha, kwani watu wa makaburi haya mawili, anaadhibiwa kila mmoja kati yao kwa dhambi aliloliacha na haliyakuwa kujiweka mbali nalo ni jambo jepesi kwa yule atakayeafikishwa na Mwenyezi Mungu kwa hilo. Mmoja kati ya hawa wanaoadhibiwa alikuwa hajichungi kutokana na mkojo wake wakati wa kukidhi haja, na wala hajihifadhi kutokana na mkojo, najisi ikampata na ikachafua mwili wake na nguo zake na wala hajisitiri wakati wa kukidhi haja, na mmoja alikuwa akitembea baina ya watu akiwafitinisha mpaka asababishe uadui na chuki baina ya watu, na hasa hasa ndugu wa karibu na marafiki, na uislamu hakika umekuja na mapenzi na muungano baina ya watu na kukata mizozo na ugomvi. Lakini mkarim mpole -Rehema na Amani ziwe juu yake- zilimpata huruma na upole kwao, akachukua tawi bichi la mtende akalipasua mara mbili, na akapanda katika kila kaburi kipande kimoja, wakamuuliza maswahaba Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kuhusu kitendo hiki kigeni kwao, Akasema: Huenda Mwenyezi Mungu atawapunguzia kwa utetezi wangu yale yanayowapata katika adhabu, katika kipindi ambacho yatakuwa hayajakauka matawi haya, yaani muda wote yatakapobaki kuwa mabichi, Na kitendo hiki ni maalumu kwake yeye -Rehema na Amani ziwe juu yake-.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya kifaransa Kiispania Kituruki Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Lugha ya Kibosnia Lugha ya Kirashia Kibangali Kichina Kifursi Kitagalogi Kihindi Kivetenamu Kisin-hala Ki ighori Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Thai Pashto Kiassam السويدية الأمهرية
Kuonyesha Tarjama