عَنْ أَبِي ذَرٍّ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ أَنَّهُ سَمِعَ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ:
«لاَ يَرْمِي رَجُلٌ رَجُلًا بِالفُسُوقِ، وَلاَ يَرْمِيهِ بِالكُفْرِ، إِلَّا ارْتَدَّتْ عَلَيْهِ، إِنْ لَمْ يَكُنْ صَاحِبُهُ كَذَلِكَ».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 6045]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abuu Dharri radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba yeye alimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema:
"Hatomtuhumu mtu mwenzake kwa machafu, na wala hatomtuhumu kwa ukafiri, isipokuwa hurejea kwake, ikiwa ndugu yake hatokuwa hivyo".
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 6045]
Ametahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakayesema kumwambia mwingine: Wewe ni muovu, au: Wewe ni kafiri, ikiwa hatokuwa kama alivyosema, basi yeye ndiye atakayestahiki sifa iliyotajwa, na kauli yake itarudi kwake, na ama akiwa kama alivyosema basi hakuna kitakachorejea kwake; kwa sababu atakuwa mkweli katika hayo aliyoyasema.