+ -

عن عائشة رضي الله عنها قالت:
كَانَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَذْكُرُ اللهَ عَلَى كُلِّ أَحْيَانِهِ.

[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 373]
المزيــد ...

Kutoka kwa Aisha -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema:
Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akimtaja Allah katika nyakati zake zote.

[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 373]

Ufafanuzi

Anaeleza Aisha mama wa waumini -Radhi za Allah ziwe juu yake- kuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alikuwa na pupa kubwa ya kumtaja Allah Mtukufu, nakuwa yeye alikuwa akimtaja Allah Mtukufu katika nyakati zote mahala popote na katika hali zote.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese Thai German Kijapani Pashto Kiassam Albanian السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية Luqadda qer-qeesiya النيبالية Luqadda yuruuba الليتوانية الدرية الصربية الصومالية Luqadda kiniya ruwadiga الرومانية المجرية التشيكية Luqadda malgaashka Kiitaliano Luqadda kinaadiga الأوكرانية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Hakuna sharti la twahara ya hadathi ndogo na kubwa kwa ajili ya kumtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu.
  2. Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- alikuwa akidumu na kumtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu.
  3. Himizo la kukithirisha kumja Mwenyezi Mungu Mtukufu katika nyakati zote kwa kumuiga Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-, isipokuwa katika hali ambazo zinakatazwa ndani yake kufanya hivyo, kama kukidhi haja.
Ziada