عَنْ أَنَسٍ رضي الله عنه أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:
«إِذَا تَوَضَّأَ أَحَدُكُمْ وَلَبِسَ خُفَّيْهِ فَلْيُصَلِّ فِيهِمَا، وَلْيَمْسَحْ عَلَيْهِمَا ثُمَّ لَا يَخْلَعْهُمَا إِنْ شَاءَ إِلَّا مِنْ جَنَابَةٍ».
[صحيح] - [رواه الدارقطني] - [سنن الدارقطني: 781]
المزيــد ...
Imepokewa kutoka kwa Anas -radhi za Allah ziwe juu yake- : Yakwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake amesema:
"Atakapotawadha mmoja wenu na akavaa khofu zake (au soksi zake) basi na aswali nazo, na afute juu yake kisha asizivue akitaka kufanya hivyo isipokuwa atakapokuwa na janaba".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Addaar- Alqutni] - [سنن الدارقطني - 781]
Anabainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa muislamu atakapovaa khofu zake baada ya kutawadha, kisha akatengukwa udhu baada ya hapo, na akataka kutawadha, basi anatakiwa afute juu yake akitaka kufanya hivyo, na aswali nazo wala asizivue kwa muda maalum, isipokuwa atakapopatwa na janaba hapo atalazimika kuvua khofu na kuoga.