عَنْ زِرِّ بْنِ حُبَيْشٍ قَالَ:
أَتَيْتُ صَفْوَانَ بْنَ عَسَّالٍ المُرَادِيَّ، أَسْأَلُهُ عَنِ المَسْحِ عَلَى الخُفَّيْنِ، فَقَالَ: مَا جَاءَ بِكَ يَا زِرُّ؟ فَقُلْتُ: ابْتِغَاءَ العِلْمِ، فَقَالَ: إِنَّ المَلاَئِكَةَ لَتَضَعُ أَجْنِحَتَهَا لِطَالِبِ العِلْمِ؛ رِضًا بِمَا يَطْلُبُ، فَقُلْتُ: إِنَّهُ حَكَّ فِي صَدْرِي المَسْحُ عَلَى الخُفَّيْنِ بَعْدَ الغَائِطِ وَالبَوْلِ، وَكُنْتَ امْرَأً مِنْ أَصْحَابِ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، فَجِئْتُ أَسْأَلُكَ: هَلْ سَمِعْتَهُ يَذْكُرُ فِي ذَلِكَ شَيْئًا؟ قَالَ: نَعَمْ، كَانَ يَأْمُرُنَا إِذَا كُنَّا سَفْرًا أَوْ مُسَافِرِينَ أَلَّا نَنْزِعَ خِفَافَنَا ثَلاَثَةَ أَيَّامٍ وَلَيَالِيهِنَّ إِلَّا مِنْ جَنَابَةٍ، لَكِنْ مِنْ غَائِطٍ وَبَوْلٍ وَنَوْمٍ، فَقُلْتُ: هَلْ سَمِعْتَهُ يَذْكُرُ فِي الهَوَى شَيْئًا؟ قَالَ: نَعَمْ، كُنَّا مَعَ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي سَفَرٍ فَبَيْنَا نَحْنُ عِنْدَهُ إِذْ نَادَاهُ أَعْرَابِيٌّ بِصَوْتٍ لَهُ جَهْوَرِيٍّ: يَا مُحَمَّدُ، فَأَجَابَهُ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَلَى نَحْوٍ مِنْ صَوْتِهِ: «هَاؤُمُ» وَقُلْنَا لَهُ: وَيْحَكَ اغْضُضْ مِنْ صَوْتِكَ، فَإِنَّكَ عِنْدَ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، وَقَدْ نُهِيتَ عَنْ هَذَا، فَقَالَ: وَاللَّهِ لاَ أَغْضُضُ، قَالَ الأَعْرَابِيُّ: المَرْءُ يُحِبُّ القَوْمَ وَلَمَّا يَلْحَقْ بِهِمْ، قَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «المَرْءُ مَعَ مَنْ أَحَبَّ يَوْمَ القِيَامَةِ»، فَمَا زَالَ يُحَدِّثُنَا حَتَّى ذَكَرَ بَابًا مِنْ قِبَلِ المَغْرِبِ مَسِيرَةُ عَرْضِهِ، أَوْ يَسِيرُ الرَّاكِبُ فِي عَرْضِهِ أَرْبَعِينَ أَوْ سَبْعِينَ عَامًا.
[صحيح] - [رواه الترمذي وابن ماجه وأحمد] - [سنن الترمذي: 3535]
المزيــد ...
Kutoka kwa Zirri bin Hubaishi amesema:
Nilikwenda kwa Swafwan bin Assali Al-Muraadi, ili nimuulize kuhusu kufuta juu ya khofu mbili, akasema: Ni nini kimekuleta ewe Zirri? Nikasema: Kutafuta elimu, akasema: Hakika Malaika huweka mbawa zao kwa mwenye kutafuta elimu; kwa kuridhishwa na kile anachokitafuta, basi nikasema: Hakika mimi nimepata uzito ndani ya kifua changu kuhusu kufuta juu ya khofu mbili baada ya kukidhi haja ndogo na kubwa, na wewe ulikuwa miongoni mwa wanafunzi wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, hivyo nimekuja kukuuliza: Je, uliwahi kumsikia akizungumza chochote kuhusu hilo? Akasema: Ndiyo, Alikuwa kituamrisha tunapokuwa safarini tusivue khofu zetu kwa siku tatu (mchana na usiku) isipokuwa kwa ajili ya janaba, lakini ni kwa haja kubwa na ndogo na usingizi, nikasema: Je, uliwahi kumsikia akizungumza chochote kuhusu matamanio? Akasema: Ndiyo, tulikuwa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika safari, wakati tukiendelea kuwa naye ghafla, Bedui mmoja alimuita kwa sauti kubwa na ya juu. Ewe Muhammadi!!!, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamjibu kwa mfano wa sauti yake: "Ehee, niambie!" Tukasema kumwambia koma!, punguza sauti yako, kwani hapa uko mbele ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na umekatazwa kufanya hivi, akasema: Wallahi siwezi kupunguza, kisha Bedui akasema: Utakuta mtu anawapenda watu fulani lakini hajawahi kukutana nao, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Mtu atakuwa pamoja na yule anayempenda siku ya Kiyama" Basi akaendelea kutusimulia mpaka akautaja mlango ulioko Magharibi mwendo wa upana wake, au anaweza kutembea aliyepanda kwenye upana wake kwa miaka arobaini au sabini.
[Sahihi] - [رواه الترمذي وابن ماجه وأحمد] - [سنن الترمذي - 3535]
Alikuja Zirri bin Hubaishi kwa Swafwan bin Assali radhi za Allah ziwe juu yake, ili amuulize kuhusu khofu mbili, Swafwan akasema: Ni nini kimekuleta ewe Zirri? Akasema: Kutafuta elimu, akasema: Hakika Malaika huweka mbawa zao kwa mwenye kutafuta elimu; kwa kuridhishwa na kutukuza kile anachokifanya mwenye kutafuta elimu, Zirii akasema: Hakika nimepata shaka ndani ya nafsi yangu kuhusu kufuta juu ya khofu mbili baada ya haja kubwa na ndogo, na wewe ni katika Maswahaba wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na nimekuja hapa kukuuliza, je, uliwahi kumsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akitaja chochote kuhusu hili?. Akasema Swafwan: Ndiyo, alikuwa akituamrisha tunapokuwa wasafiri tusivue khofu zetu kwa siku tatu (mchana na usiku) kwa sababu ya hadathi (uchafu) mdogo, kama haja kubwa na ndogo na usingizi, isipokuwa janaba hapo basi ni wajibu kuvua, nikasema: Je, uliwahi kumsikia akizungumza chochote kuhusu mapenzi? Akasema: Ndiyo: Tulikuwa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika safari, wakati tukiwa bado tuko pamoja naye mara ghafla Bedui mmoja aliita kwa sauti ya juu sana: Ewe Muhammadi!, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamjibu kwa sauti ya juu karibu na sauti yake: Njoo, nasi tukasema kumwambia: Koma! Shusha sauti yako, kwani hapa uko mbele ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na umekatazwa kunyanyua sauti mbele yake. Akasema kwa sababu ya ukaidi wake: Wallahi siwezi kuishusha, Bedui akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, utakuta mtu anawapenda watu wema na hajafanya matendo mfano wa matendo yao? Akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Mtu atakuwa pamoja na anayempenda siku ya Kiyama, Anasema Zirri: Swafwan akaendelea kutuhadithia mpaka akataja mlango wa toba ulioko upande wa Sham aliuumba Mwenyezi Mungu siku aliyoumba Mbingu na Ardhi, anaweza kutembea aliyepanda juu ya kipando kwenye upana wake miaka arobaini au sabini, na wala haufungwi mpaka Jua lichomoze kutokea Magharibi yake.