عَنْ أَبِي الحَوْرَاءِ السَّعْدِيِّ قَالَ: قُلْتُ لِلْحَسَنِ بْنِ عَلِيٍّ رضي الله عنهما: مَا حَفِظْتَ مِنْ رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ؟ قَالَ: حَفِظْتُ مِنْ رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«دَعْ مَا يَرِيبُكَ إِلَى مَا لاَ يَرِيبُكَ، فَإِنَّ الصِّدْقَ طُمَأْنِينَةٌ، وَإِنَّ الكَذِبَ رِيبَةٌ».
[صحيح] - [رواه الترمذي والنسائي وأحمد] - [سنن الترمذي: 2518]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abul Hauraai Assa'di amesema: Nilisema kumwambia Hassan bin Ally radhi za Allah ziwe juu yao: Ulihifadhi nini kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake? Akasema: Nilihifadhi kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake?
"Acha linalokutia shaka fanya lisilokutia shaka, kwani ukweli ni utulivu, na bila shaka uongo ni shaka"
[Sahihi] - - [سنن الترمذي - 2518]
Aliamrisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuacha kile ulicho na shaka nacho katika maneno na matendo nakuwa jambo hilo limekatazwa toka mwanzo, je jambo hili ni halali au ni haramu, afanye asilo na shaka nalo katika yale ambayo anaamini kuwa ni mazuri na ni halali, kwa sababu moyo unatulizana na unatulia katika hilo, na hakuna shaka ndani yake inayotia msongo na taharuki.