عَنْ المُغِيرَةِ رضي الله عنه قَالَ:
كُنْتُ مَعَ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي سَفَرٍ، فَأَهْوَيْتُ لِأَنْزِعَ خُفَّيْهِ، فَقَالَ: «دَعْهُمَا، فَإِنِّي أَدْخَلْتُهُمَا طَاهِرَتَيْنِ» فَمَسَحَ عَلَيْهِمَا.
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 206]
المزيــد ...
Kutoka kwa MughIira Radhi za Allah ziwe juu yake amesema:
Nilikuwa pamoja na Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- katika safari, nikanyoosha mikono ili nimvue viatu vyake (khufu), akasema: "Ziache, kwani hakika mimi nimezivaa zikiwa safi", akafuta juu yake.
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 206]
Alikuwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- katika moja ya safari zake akatawadha, alipofikia kuosha miguu miwili alinyoosha Mughira bin Shu'ba Radhi za Allah ziwe juu yake mikono yake ili avue kilichokuwa miguuni kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- katika khufu (viatu mithili ya soksi) ili Mtume aoshe miguu yake! Akasema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: Ziache na wala usizivue, kwani mimi niliingiza miguu yangu ndaniya khufu mbili nikiwa katika twahara, Akafuta Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- juu ya khufu zake badala ya kuosha miguu miwili.