+ -

عَنْ جَابِرٍ رضي الله عنه قَالَ: سَمِعْتُ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ:
«إِنَّ الشَّيْطَانَ قَدْ أَيِسَ أَنْ يَعْبُدَهُ الْمُصَلُّونَ فِي جَزِيرَةِ الْعَرَبِ، وَلَكِنْ فِي التَّحْرِيشِ بَيْنَهُمْ».

[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 2812]
المزيــد ...

Imepokelewa kutoka kwa Jabiri -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- akisema:
"Hakika shetani alishakata tamaa kuabudiwa na wenye kuswali katika kisiwa cha Arab, Lakini yuko katika kuwachochea baina yao".

[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 2812]

Ufafanuzi

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa Ibilisi amekwishakata tamaa waumini wenye kuswali kurudi kuabudu na kusujudia masanamu katika kisiwa Arab, lakini bado anatamaa, na bado nguvu zake na juhudi zake na harakati zake ziko katika kuwachochea baina yao kwa ugomvi na chuki na vita na fitina na mfano wa hayo.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Pashto Kiassam الأمهرية الهولندية الغوجاراتية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Kumuabudu Shetani ni kuabudu sanamu, kwa sababu yeye ndiye muamrishaji na mshawishi wa hilo, kwa dalili ya kauli yake Mtukufu kuhusu Nabii Ibrahim -amani iwe juu yake- (aliposema): "Ewe baba yangu usimuabudu Shetani...."
  2. Shetani anakwenda mbio katika kuchochea ugomvi na chuki na vita na fitina baina ya waislamu.
  3. Miongoni mwa faida za swala katika Uislamu nikuwa inalinda mapenzi kati ya waislamu, na ikayatia nguvu mahusiano ya kiudugu baina yao.
  4. Swala ndiyo nembo kubwa ya dini baada ya shahada mbili, na ndio maana wameitwa waislamu wanaoswali.
  5. Kisiwa Arab kina mambo maalumu yasiyokuwepo katika miji mingine.
  6. Ikiwa kutasema kuwa, mbona kumetokea katika baadhi ya Kisiwa Arab ibada za masanamu, hali yakuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake anasema: "Hakika Shetani amekwishakata tamaa ya kuabudiwa na wenye kuswali...", hii ni taarifa ya yale yaliyotokea katika nafsi ya Shetani katika kukata tamaa baada ya kuona ufunguzi wa miji mbali mbali, na watu kuingia ndani ya dini ya Mwenyezi Mungu makundi kwa makundi, hadithi imeeleza dhana ya Shetani na kutokea kwake, kisha uhalisia ukawa kinyume na matarajio kwa hekima aliyoitaka Mwenyezi Mungu Mtukufu.