+ -

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:
«مَنْ تَرَدَّى مِنْ جَبَلٍ فَقَتَلَ نَفْسَهُ فَهُوَ فِي نَارِ جَهَنَّمَ يَتَرَدَّى فِيهِ خَالِدًا مُخَلَّدًا فِيهَا أَبَدًا، وَمَنْ تَحَسَّى سُمًّا فَقَتَلَ نَفْسَهُ فَسُمُّهُ فِي يَدِهِ يَتَحَسَّاهُ فِي نَارِ جَهَنَّمَ خَالِدًا مُخَلَّدًا فِيهَا أَبَدًا، وَمَنْ قَتَلَ نَفْسَهُ بِحَدِيدَةٍ فَحَدِيدَتُهُ فِي يَدِهِ يَجَأُ بِهَا فِي بَطْنِهِ فِي نَارِ جَهَنَّمَ خَالِدًا مُخَلَّدًا فِيهَا أَبَدًا».

[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 5778]
المزيــد ...

Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema:
"Atakayejirusha kutoka juu ya mlima akajiua basi huyo atakuwa motoni akijirusha humo milele na milele, na atakayemeza sumu akajiua basi sumu yake itakuwa mkononi mwake akiimeza ndani ya Moto wa Jahannamu milele na milele humo, na atakayeiua nafsi yake kwa chuma basi chuma chake kitakuwa mkono mwake akilichomo tumbo lake ndani ya Moto Jahannamu milele na milele humo".

[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 5778]

Ufafanuzi

Ametahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa yeyote atakayekusudia kujiua katika dunia, basi ataadhibiwa siku ya Kiyama ndani ya Moto wa Jahannamu kwa njia hiyo hiyo aliyoifanya yeye mwenyewe katika dunia, hayo yakiwa ni malipo kulingana na alichokifanya, atakayejirusha mwenyewe kutoka juu ya mlima akajiua, basi atakuwa ndani ya Moto wa Jahannam akidondoka humo katika milima ya Jahannamu na katika mabonde yake milele na mile humo, na atakayejipiga mwenyewe kwa chuma tumboni mwake akajiua, basi chuma chake kitakuwa mkononi kwake akichoma kwa chuma hicho tumbo lake ndani ya Moto wa Jahannam milele na milele humo.

Tafsiri: Lugha ya Kiindonesia Kivetenamu Kiassam الهولندية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Uharamu wa mtu kujiua mwenyewe, na kwamba hilo ni katika madhambi makubwa ambayo mtu anastahiki adhabu kali kwa hilo.
  2. Yaliyotajwa katika hadithi ni baadhi ya aina za kujitoa uhai, na vinginevyo, kwa njia yoyote atakayojiua mtu ataadhibiwa kwa mfano wa kile alichokifanya, na imekuja katika Sahihi Bukhari kauli yake rehema na amani ziwe juu yake: "Anayejinyonga mwenyewe basi anainyonga nafsi yake katika Moto, na anayejichoma kwa kitu chenye ncha kali basi anaichoma nafsi yake katika Moto".
  3. Amesema Nawawi: Na ama kauli yake rehema na amani ziwe juu yake: "Basi atakuwa katika Moto wa Jahannam milele na milele humo"; Kumesemwa ndani yake kauli nyingi: Ya kwanza: Nikuwa hili linachukuliwa hivyo kwa atakayefanya hivyo kwa kuhalalisha kitendo hicho huku akijua uharamu wake, basi huyu ni kafiri, na hii ndiyo adhabu yake. Ya pili: Nikuwa makusudio ya milelel ni kukaa muda mrefu na maisha marefu na si uhalisia wa kuishi milele, kama inavyoweza kusemwa: Mwenyezi Mungu aubakishe milele ufalme wa mfalme. Na ya tatu: Ni kuwa haya ni malipo yake, lakini kwa takrima ya Aliyetakasika na kutukuka alieleza kuwa hatombakisha milele yeyote atakayekufa akiwa ni muislamu.
  4. Hii ni katika sehemu ya adhabu za Akhera kuendana na aina ya makosa ya duniani, na inachukuliwa katika hili kuwa kosa la jinai la mtu kwa nafsi yake ni kama kumtendea jinai mtu mwingine kulingana na madhambi yake; kwa sababu nafsi yake si milki yake moja kwa moja, bali ni milki ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, hivyo, hawezi kuwa na maamuzi yoyote isipokuwa yale yaliyoidhinishwa kwake.