عَنِ ابْنِ عُمَرَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«لَنْ يَزَالَ المُؤْمِنُ فِي فُسْحَةٍ مِنْ دِينِهِ، مَا لَمْ يُصِبْ دَمًا حَرَامًا».
[صحيح] - [رواه البخاري] - [صحيح البخاري: 6862]
المزيــد ...
Kutoka kwa bin Omari -radhi za Allah ziwe juu yake yeye na baba yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-:
"Muumini hatoacha kuendelea kuwa katika wigo mpana katika dini yake, madam hajagusa damu ya haramu".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Al-Bukhaariy] - [صحيح البخاري - 6862]
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba muumini huendelea kuwa katika nafasi pana ya matendo mema, na kutaraji rehema ya Mwenyezi Mungu na msamaha na maghufira yake, mpaka atakapouwa mtu aliyeharamishwa kuuawa basi amali zake zitakuwa nyembamba kwake; kwa sababu hazitoshelezi kulipa mauaji na dhambi lake kubwa.