+ -

عَن أَبي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه عَنِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:
«لاَ يُشِيرُ أَحَدُكُمْ عَلَى أَخِيهِ بِالسِّلاَحِ، فَإِنَّهُ لاَ يَدْرِي، لَعَلَّ الشَّيْطَانَ يَنْزِعُ فِي يَدِهِ، فَيَقَعُ فِي حُفْرَةٍ مِنَ النَّارِ».

[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 7072]
المزيــد ...

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema:
"Asiashirie mmoja wenu silaha kwa ndugu yake, kwani hajui, huenda Shetani akaipokonya kutoka mkononi mwake, akatumbukia katika shimo la moto".

[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 7072]

Ufafanuzi

Ametahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake muislamu kuashiria juu ya ndugu yake muislamu kwa silaha, kwa aina yoyote ile miongoni mwa aina za silaha, kwa sababu yeye hajui huenda Shetani akamsukuma kuitikisa silaha mkononi mwake, akamuuwa ndugu yake au akamuudhi, akatumbukia katika maasi yanayoweza kumpelekea kuingia katika shimo la moto.

Tafsiri: Lugha ya Kiindonesia Kivetenamu Kihausa Kiassam الأمهرية الهولندية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Kumebainishwa uharamu wa damu muislamu.
  2. Ulazima wa kumheshimu muislamu na tahadhari ya kumfikishia shari kwake kwa kitendo au kauli, ikiwemo kumuashiria kwa chuma au silaha, hata kama ni kwa mzaha; kwa sababu Shetani anaweza kuutelezesha mkono wake na akampendezeshea kumpiga ndugu yake, au akaipokonya silaha kutoka mkononi mwake ikatua pasina maamuzi yake ikamdhuru ndugu yake.
  3. Kuziba njia zinazopelekea katika jambo kwa kukataza yanayopelekea katika haramu.
  4. Pupa ya kuhakikisha usalama wa jamii na kuhifadhi mahusiano baina ya watu, na kutowatisha na kuwaogopesha hata kama ni kwa ishara na kutishia.