عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: مَا خَطَبَنَا نَبِيُّ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِلَّا قَالَ:
«لَا إِيمَانَ لِمَنْ لَا أَمَانَةَ لَهُ، وَلَا دِينَ لِمَنْ لَا عَهْدَ لَهُ».
[حسن لغيره] - [رواه أحمد] - [مسند أحمد: 12383]
المزيــد ...
Kutoka kwa Anasi bin Maliki radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Hakuwahi kutuhutubia sisi Mtume rehema na amani ziwe juu yake isipokuwa alisema:
"Hana imani asiyekuwa na uaminifu, na hana dini asiyekuwa na ahadi (za kweli)".
[Ni nzuri kwa sababu ya hadithi nyingine] - [Imepokelewa na Ahmad] - [مسند أحمد - 12383]
Anaeleza Anasi bin Maliki radhi za Allah ziwe juu yake kuwa ni mara chache sana akihutubia Mtume rehema na amani ziwe juu yake au atoe mawaidha isipokuwa alikuwa akitaja mambo mawili: La kwanza: Hana imani mtu ambaye ndani ya nafsi yake kuna hiyana na mtu katika mali yake au nafsi yake au familia yake. La pili: Hana dini kamili mwenye kufanya hiyana katika ahadi na mikataba na kuivunja.