عَنْ أَبِي الدَّرْدَاءِ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«أَلاَ أُخْبِرُكُمْ بِأَفْضَلَ مِنْ دَرَجَةِ الصِّيَامِ وَالصَّلاَةِ وَالصَّدَقَةِ؟» قَالُوا: بَلَى، قَالَ: «صَلاَحُ ذَاتِ البَيْنِ، فَإِنَّ فَسَادَ ذَاتِ البَيْنِ هِيَ الحَالِقَةُ».
[صحيح] - [رواه أبو داود والترمذي] - [سنن الترمذي: 2509]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abuu Dardai -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake:
"Hivi nisikuelezeni lililo bora kuliko daraja ya swaumu na swala na sadaka?" Wakasema: Tueleze, akasema: "Kusuluhisha kati ya watu, kwani kuharibika kwa mahusiano baina ya watu hilo hunyoa".
[Sahihi] - [رواه أبو داود والترمذي] - [سنن الترمذي - 2509]
Aliwauliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake Maswahaba zake: Je, nikuelezeni lililo bora kuliko kuzidisha ibada za sunna kama swaumu na swala na sadaka? Wakasema: Ndio. Akasema: Ni kuwapatanisha waliogombana kwani ugomvi huleta mfarakano na kujitenga na kuchukiana na kupeana migongo kati ya watu, kwani yanayoambatana na kuharibika kwa mahusiano baina ya watu miongoni mwa chuki ndio jambo ambalo katika tabia zake huangamiza na kuing'oa dini na dunia kama wembe unavyong'oa nywele.