عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«إِنَّ اللهَ يَرْضَى لَكُمْ ثَلَاثًا، وَيَكْرَهُ لَكُمْ ثَلَاثًا، فَيَرْضَى لَكُمْ: أَنْ تَعْبُدُوهُ، وَلَا تُشْرِكُوا بِهِ شَيْئًا، وَأَنْ تَعْتَصِمُوا بِحَبْلِ اللهِ جَمِيعًا وَلَا تَفَرَّقُوا، وَيَكْرَهُ لَكُمْ: قِيلَ وَقَالَ، وَكَثْرَةَ السُّؤَالِ، وَإِضَاعَةِ الْمَالِ».
[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 1715]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-:
"Hakika Mwenyezi Mungu anaridhia kwenu mambo matatu, na anachukia kwenu mambo matatu, basi anaridhia kwenu: Mumuabudu yeye, na wala msimshirikishe na chochote, na mshikamane katika kamba ya Mwenyezi Mungu nyote na wala msifarakane, na anachukia kwenu mambo matatu: Umbeya, na kuuliza uliza sana, na kupoteza mali".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 1715]
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba Mwenyezi Mungu anapenda kwa waja wake mambo matatu, na anachukia kutoka kwao mambo matatu, anapenda kutoka kwao: Wampwekeshe yeye pekee na wala wasimshirikishe na chochote, na washikamane na ahadi ya Mwenyezi Mungu na Qur'ani na mafundisho ya Nabii wake wote, na wala wasifarakane katika umoja wa Waislamu. Na anachukia kwao: Upuuzi na maneno yasiyokuwa na faida katika yale yasiyowahusu, na kuuliza jambo ambalo bado halijatokea, au kuwaomba watu mali zao, na vile wanavyovimiliki, na yale yasiyokuwa na ulazima wa kuyaomba, na kupoteza mali na kuzitumia katika njia zisizokuwa za kisheria, na kuziweka katika uharibifu.