+ -

عَنْ عُمَرَ بْنِ الخَطَّابِ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ:
أَنَّ رَجُلًا عَلَى عَهْدِ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَانَ اسْمُهُ عَبْدَ اللَّهِ، وَكَانَ يُلَقَّبُ حِمَارًا، وَكَانَ يُضْحِكُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، وَكَانَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَدْ جَلَدَهُ فِي الشَّرَابِ، فَأُتِيَ بِهِ يَوْمًا فَأَمَرَ بِهِ فَجُلِدَ، فَقَالَ رَجُلٌ مِنَ القَوْمِ: اللَّهُمَّ الْعَنْهُ، مَا أَكْثَرَ مَا يُؤْتَى بِهِ؟ فَقَالَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «لاَ تَلْعَنُوهُ، فَوَاللَّهِ مَا عَلِمْتُ أَنَّهُ يُحِبُّ اللَّهَ وَرَسُولَهُ».

[صحيح] - [رواه البخاري] - [صحيح البخاري: 6780]
المزيــد ...

Imepokelewa kutoka kwa Omari bin Khattwab -radhi za Allah ziwe juu yake-:
Ya kwamba mtu mmoja alikuwa katika zama za Mtume rehema na amani ziwe juu yake jina lake anaitwa Abdallah, na alikuwa akitaniwa kwa jina la Punda, na alikuwa akimchekesha Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake amekwisha mchapa viboko kwa sababu ya ulevi, basi akaletwa siku moja akaamrisha akachapwa, akasema mtu mmoja katika jamaa waliopo: Ewe Mwenyezi Mungu mlaani, ni mara ngapi analetwa!? Akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Msimlaani, Wallahi, namuapa Mwenyezi Mungu sikujua lolote kwake isipokuwa anampenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake".

[Sahihi] - [Imepokelewa na Al-Bukhaariy] - [صحيح البخاري - 6780]

Ufafanuzi

Katika zama za Mtume rehema na amani ziwe juu yake kulikuwa na bwana mmoja jina lake Abdallah, na akiitwa Punda, kwa jina la utani, na alikuwa akimchekesha sana Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika baadhi ya maneno yake, na alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake amekwisha mchapa kwa sababu ya kunywa pombe, siku moja akaletwa tena akiwa amekunywa pombe, akaamrisha akachapwa. Mmoja kati ya waliopo akamtukana, na akasema: Mwenyezi Mungu mlaani, amezidi sana kuletwa kwa sababu ya kunywa pombe?! Akasema rehema na amani ziwe juu yake: Msimuombee kufukuzwa katika rehema ya Mwenyezi Mungu, na Wallahi sijajua lolote kwake isipokuwa anampenda Mwenyezi Mungu na Mtume.

Katika Faida za Hadithi

  1. Haipingani kati ya kufanya makatazo na kuthibiti kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake ndani ya moyo wa mwenye kuyafanya; kwa sababu yeye rehema na amani ziwe juu yake ameeleza kuwa huyo aliyetajwa katika hadithi anampenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake pamoja na hayo yaliyojitokeza kwake.
  2. Mtenda madhambi makubwa atakapokufa na huku anaendelea na chochote katika hayo huyo atakuwa chini ya matashi, akitaka Mwenyezi Mungu atamsamehe na akitaka atamuadhibu, na habakishwi milele motoni yeyote katika Waislamu.
  3. Inachukiza kumlaani mnywa pombe; kwa kutaraji kuwa huenda kukawa na kizuizi cha kutompata laana; kwa sababu kumlaani mtu maalumu na kumuombea dua mbaya, huenda hilo likampelekea katika ujeuri, au likamkatisha tamaa ya kukubaliwa toba.
  4. Inafaa kulaani bila kumuanisha mtu kwa hilo.
Tafsiri: Lugha ya Kiindonesia Kibangali Kivetenamu Kikurdi Kireno Thai Kiassam الهولندية الدرية المجرية الجورجية المقدونية
Kuonyesha Tarjama