+ -

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«بَدَأَ الْإِسْلَامُ غَرِيبًا، وَسَيَعُودُ كَمَا بَدَأَ غَرِيبًا، فَطُوبَى لِلْغُرَبَاءِ».

[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 145]
المزيــد ...

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-:
"Ulianza Uislamu ukiwa ni mgeni na utarudi kuwa mgeni kama ulivyo anza, basi shangwe kwa wale wanaoonekana kuwa ni wageni".

[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 145]

Ufafanuzi

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba Uislamu ulianza ukiwa kwa mtu mmoja mmoja na uchache wa watu wake, na utarejea ukiwa mgeni kwa uchache wa wenye kuutekeleza kama ulivyoanza, twawatamani, na uzuri ulioje kwa wageni, na furaha na kitulizo cha jicho kwao.

Tafsiri: Lugha ya Kiindonesia Kivetenamu Kiassam الهولندية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Habari kuhusu kutokea ugeni wa Uislamu baada ya kuenea kwake na umaarufu wake.
  2. Hapa kuna alama miongoni mwa alama za utume, kiasi kwamba ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake yale yatakayotokea baada yake, na ikatokea kama alivyoeleza.
  3. Fadhila ya atakayehama nchi yake na familia yake; na kwamba atakuwa na Pepo.
  4. Wageni ni wale wanaotengemaa watu wanapoharibika, nao ni wale wanaorekebisha yale waliyoyaharibu watu.