+ -

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ:
«لاَ يَزَالُ قَلْبُ الكَبِيرِ شَابًّا فِي اثْنَتَيْنِ: فِي حُبِّ الدُّنْيَا وَطُولِ الأَمَلِ».

[صحيح] - [رواه البخاري] - [صحيح البخاري: 6420]
المزيــد ...

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- akisema:
"Moyo wa mzee huendelea kuwa kijana katika mambo mawili: Katika kupenda dunia na matumaini ya muda mrefu".

[Sahihi] - [Imepokelewa na Al-Bukhaariy] - [صحيح البخاري - 6420]

Ufafanuzi

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa mzee huzeeka na mwili wake kudhoofika, lakini moyo wake huwa kijana kwa kupenda mambo mawili: La kwanza: Kuipenda dunia kwa kuwa na wingi wa mali. La pili: Kuwa na uhai na maisha na umri na matarajio ya muda mrefu.

Katika Faida za Hadithi

  1. Kumebainishwa tabia alioumbwa nayo mwanadamu, nayo ni kuipenda dunia na matumaini marefu.
  2. Hapa kuna ishara ya kuonyesha ubaya wa kuwa na matumaini ya muda mrefu, na pupa ya kukusanya mali, na hilo linachochea kujiandaa na kifo na ubora wa kutoa sadaka kwa mwenye uwezo, na masikini kujizuia kuomba.
  3. Mambo yanayopendeka zaidi kwa mwanadamu ni nafsi yake, kwani anatamani iendelee kubakia, akapenda kwa hilo kuwa na umri mrefu, na akapenda mali; kwa sababu ni katika sababu kubwa za kudumu kwa afya na starehe, kila anapohisi kukaribia kumalizika kwa hilo basi mapenzi yanazidi kuwa makubwa, na hamu yake ya kutamani idumu inaongezeka.
Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiindonesia Kisin-hala Kivetenamu Kihausa Kiassam الهولندية الغوجاراتية الرومانية المجرية الجورجية
Kuonyesha Tarjama