+ -

عَنْ سَهْلِ بْنِ سَعْدٍ رَضيَ اللهُ عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«إِيَّاكُمْ وَمُحَقَّرَاتِ الذُّنُوبِ، فَإِنَّمَا مَثَلُ مُحَقَّرَاتِ الذُّنُوبِ كَقَوْمٍ نَزَلُوا فِي بَطْنِ وَادٍ، فَجَاءَ ذَا بِعُودٍ، وَجَاءَ ذَا بِعُودٍ، حَتَّى أَنْضَجُوا خُبْزَتَهُمْ، وَإِنَّ مُحَقَّرَاتِ الذُّنُوبِ مَتَى يُؤْخَذْ بِهَا صَاحِبُهَا تُهْلِكْهُ».

[صحيح] - [رواه أحمد] - [مسند أحمد: 22808]
المزيــد ...

Kutoka kwa Sahal bin Sa'di Allah amridhie amesema: Amesema Mtume wa Allah rehema na amani ziwe juu yake:
"Tahadharini na madhambi yenye kudharauliwa, kwani mfano wa madhambi yenye kudharauliwa, ni kama watu walioshuka chini ya bonde, akaja huyu na kijiti, na yule na kijiti, na akaja huyu na kijiti, mpaka wakaivisha mkate wao, na bila shaka madhambi yadharauliwayo akihesabiwa mfanyaji wake yanamuangamiza".

[Sahihi] - [Imepokelewa na Ahmad] - [مسند أحمد - 22808]

Ufafanuzi

Ametahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake na kupuuza katika kuyafanya madhambi madogo, na kuyakithirisha kwani yanaangamiza yanapokuwa mengi, na akapiga mfano juu ya hilo wa watu walioshuka chini ya bonde, basi akaja kila mmoja wao na kijiti kidogo, mpaka wakaivisha mkate wao kwa mkusanyiko wa vile walivyovikusanya katika vijiti, na hakika madhambi yadharauliwayo pindi anapohesabiwa mfanyaji wake na akawa hajatubia kutokana na madhambi hayo au Mwenyezi Mungu amsamehe, basi humuangamiza.

Tafsiri: Lugha ya Kiindonesia Kivetenamu Kiassam الهولندية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Muongozo wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika kupiga mifano ili kusogeza maana karibu ili kufahamika vizuri na kuongeza ubainifu zaidi.
  2. Tahadhari ya madhambi madogo yenye kudharauliwa, na himizo la kwenda mbio ili kuyafuta.
  3. Madhambi yenye kudharauliwa yanabeba maana nyingi: Maana ya kwanza: Ni yale anayoyafanya mja miongoni mwa madhambi, akidhani kuwa ni katika madhambi madogo, hali yakuwa ni katika madhambi makubwa mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Ya pili: Ni yale anayoyafanya mja pasina kujali, na bila kutubia, yakakusanyika juu yake haya madogo mpaka yakamuangamiza. Na ya tatu: Ni yale anayoyafanya mja katika madhambi madogo, na asiyajali, yakawa ni sababu ya kutumbukia katika madhambi makubwa na yakamuangamiza.