+ -

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«أَكْثِرُوا ذِكْرَ هَادمِ اللَّذَّاتِ» يَعْنِي الْمَوْتَ.

[حسن] - [رواه الترمذي والنسائي وابن ماجه] - [سنن ابن ماجه: 4258]
المزيــد ...

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-:
"Zidisheni sana kukikumbuka kikata ladha" Yaani: Kifo.

[Ni nzuri] - - [سنن ابن ماجه - 4258]

Ufafanuzi

Amehimiza Mtume rehema na amani ziwe juu yake juu ya kukithirisha kukikumbuka kifo ambacho kukikumbuka kwake mtu anakumbuka Akhera, na kunabomoa mapenzi yake ya kupenda ladha za dunia ndani ya moyo wake, na hasa hasa zile za haramu.

Katika Faida za Hadithi

  1. Kifo kinakata ladha za dunia, lakini kwa muumini kinamuhamisha kwenda katika ladha za Akhera na ladha za pepo na yale yanayopatikana ndani yake miongoni mwa kheri kubwa.
  2. Kukumbuka kifo na yale yanayokuwa baada yake ni miongoni mwa sababu za kutubia na kujiondoa katika dhambi na kujiandaa na Akhera.
Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiindonesia Kisin-hala Kivetenamu Kihausa Kiassam الهولندية الغوجاراتية الرومانية المجرية الجورجية
Kuonyesha Tarjama