عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عُمَرَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا:
أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ وَهُوَ عَلَى المِنْبَرِ، وَذَكَرَ الصَّدَقَةَ، وَالتَّعَفُّفَ، وَالمَسْأَلَةَ: «اليَدُ العُلْيَا خَيْرٌ مِنَ اليَدِ السُّفْلَى، فَاليَدُ العُلْيَا: هِيَ المُنْفِقَةُ، وَالسُّفْلَى: هِيَ السَّائِلَةُ».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 1429]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Abdallah bin Omari -radhi za Allah ziwe juu yake na baba yake-:
Ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alisema huku akiwa juu ya Mimbari, na akataja sadaka, na kujizuia kuomba, na kuombaomba: "Mkono wa juu ni bora kuliko mkono wa chini, mkono wa juu: Ni ule unaotoa, na mkono wa chini: Ni ule unaoomba".
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 1429]
Mtume rehema na amani ziwe juu yake alitaja sadaka, na kujizuia kuombaomba, aliyasema hayo wakati akihutubia katika Mimbari; kisha akasema: Mkono wa juu wenye kutoa sadaka ni bora na unapendeka zaidi kwa Mwenyezi Mungu kuliko mkono wa chini wenye kuomba.