+ -

عَنْ خُرَيْمِ بْنِ فَاتِكٍ رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«الْأَعْمَالُ سِتَّةٌ، وَالنَّاسُ أَرْبَعَةٌ، فَمُوجِبَتَانِ، وَمِثْلٌ بِمِثْلٍ، وَحَسَنَةٌ بِعَشْرِ أَمْثَالِهَا، وَحَسَنَةٌ بِسَبْعِ مِائَةٍ، فَأَمَّا الْمُوجِبَتَانِ: فَمَنْ مَاتَ لَا يُشْرِكُ بِاللهِ شَيْئًا دَخَلَ الْجَنَّةَ، وَمَنْ مَاتَ يُشْرِكُ بِاللهِ شَيْئًا دَخَلَ النَّارَ، وَأَمَّا مِثْلٌ بِمِثْلٍ: فَمَنْ هَمَّ بِحَسَنَةٍ حَتَّى يَشْعُرَهَا قَلْبُهُ، وَيَعْلَمَهَا اللهُ مِنْهُ كُتِبَتْ لَهُ حَسَنَةً، وَمَنْ عَمِلَ سَيِّئَةً، كُتِبَتْ عَلَيْهِ سَيِّئَةً، وَمَنْ عَمِلَ حَسَنَةً فَبِعَشْرِ أَمْثَالِهَا، وَمَنْ أَنْفَقَ نَفَقَةً فِي سَبِيلِ اللهِ فَحَسَنَةٌ بِسَبْعِ مِائَةٍ، وَأَمَّا النَّاسُ، فَمُوَسَّعٌ عَلَيْهِ فِي الدُّنْيَا مَقْتُورٌ عَلَيْهِ فِي الْآخِرَةِ، وَمَقْتُورٌ عَلَيْهِ فِي الدُّنْيَا مُوَسَّعٌ عَلَيْهِ فِي الْآخِرَةِ، وَمَقْتُورٌ عَلَيْهِ فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ، وَمُوَسَّعٌ عَلَيْهِ فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ».

[حسن] - [رواه أحمد] - [مسند أحمد: 18900]
المزيــد ...

Imepokelewa kutoka kwa Khuraimu Bin Faatik -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake-:
"Matendo yapo ya aina sita na watu wapo wako aina nne, basi kuna watu wa aina mbili wanaostahiki malipo, na malipo yao huwa sawa na matendo yao, na jema moja hulipwa kwa kumi mfano wake, na jema moja huzidishwa mpaka kufikia mema mia saba, Basi wawili wenye kustahiki malipo ni: Yeyote atakaye kufa hali yakuwa hajamshirikisha Mwenyezi Mungu na kitu chochote ataingia Peponi, na atakaye kufa hali ya kumshirikisha Mwenyezi Mungu na kitu chochote basi ataingia Motoni, na ama yule ambaye atalipwa kwa namna alivyokusudia ni yeyote atakaye kusudia kufanya jambo jema mpaka moyo wake ukahisi kuwa umetenda na Mwenyezi Mungu akajua kutenda kwake huko basi mtu huyo ataandikiwa jema moja, na atakaye fanya kosa ataandikiwa kosa moja, na atakaye fanya jema moja basi hulipwa kwa kumi mfano wake, na mwenye kutoa chochote katika njia ya Mwenyezi Mungu, basi atalipwa kwa kila kimoja kwa mara mia saba, ama watu walivyogawanyika kuna miongoni mwao waliokunjuliwa mambo yao hapa Duniani na wakawa na maisha duni huko Akhera, na kuna wenye maisha Duni hapa duniani na wakakunjuliwa maisha yao huko Akhera, na kuna wenye maisha duni hapa duniani na pia Akhera, na wakakunjuliwa maisha yao hapa duniani na kesho Akhera."

[Ni nzuri] - [Imepokelewa na Ahmad] - [مسند أحمد - 18900]

Ufafanuzi

Alieleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa matendo yapo aina sita, na watu wamegawanyika katika makundi manne, nayo ni:
Kundi la kwanza: Yeyote atakaye kufa na hakumshirikisha Mwenyezi Mungu na kitu chochote anastahiki kuingia peponi.
Kundi la pili: Yeyote atakaye kufa hali yakuwa anamshirikisha Mwenyezi Mungu na kitu kingine anastahiki kuingia motoni na atakaa humo milele.
Na matendo hayo mawili ndiyo haki mbili za msingi.
Kundi la tatu: Kukusudia kufanya wema, basi yeyote atakaye kusudia kufanya jema na akawa mkweli katika makusudio yake mpaka akahisi kweye moyo wake kuwa hili ndilo kusudio langu, kisha likamtokea jambo la kumzuia asifanye alichokikusudia katika wema huu, basi huandikiwa thawabu za wema kamili.
Kundi la nne: Kufanya tendo baya; Yeyote atakaye fanya tendo baya basi huandikiwa kosa moja.
Na matendo hayo mawili: Ndiyo hulipwa sawa sawa bila ya kuzidisha.
Kundi la Tano: Jema moja hulipwa kwa kumi mfano wake, na malipo hayo ni kwa mwenye kukusudia kufanya wema na akaufanya wema huo, basi huandikiwa mema kumi.
kundi la sita: Jema moja hulipwa sawa na mema mia saba, na malipo hayo ni kwa mwenye kutoa kitu kimoja katika njia ya Mwenyezi Mungu, basi hulipwa kwa kitu hiki kimoja kwa mema mia saba, na haya ni kutokana na fadhila za Mwenyezi Mungu aliyetakasika na Kutukuka, na ukarimu wake kwa waja wake.
Ama aina Nne ya watu ni hawa:
Aina ya kwanza: Ni mtu ambaye amekunjuliwa mambo yake hapa Duniani kwa upande wa riziki, ananeemeka humo na hupata akitakacho, lakini ni mwenye dhiki na tabu kubwa Akhera na mwisho wake ni kuingia motoni, na huyo ni tajiri wa kikafiri.
Aina ya pili: Ni mtu mwenye dhiki hapa Duniani upande wa riziki, lakini amekunjuliwa huko Akhera, na mwisho wake ni kuingia Motoni, na huyo ni muumini fakiri.
Aina ya tatu: Ni mtu mwenye dhiki hapa Duniani na Akhera, naye ni kafiri fukara.
Aina ya nne: Ni mtu aliyekunjuliwa mambo yake hapa Duniani na Akhera, naye ni muumini tajiri.

Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Burmese Thai German Pashto Kiassam Albanian السويدية الأمهرية الهولندية الغوجاراتية Luqadda qer-qeesiya النيبالية Luqadda yuruuba الليتوانية الدرية الصربية الطاجيكية Luqadda kiniya ruwadiga الرومانية المجرية التشيكية Luqadda malgaashka Kiitaliano Luqadda Oromaha Luqadda kinaadiga Luqadda Asariga الأوزبكية الأوكرانية
Kuonyesha Tarjama

Katika Faida za Hadithi

  1. Ukubwa wa fadhila za Mwenyezi Mungu kwa waja wake na kuwazidishia mambo mema.
  2. Uadilifu wa Mwenyezi Mungu na ukarimu wake, pale alipo amiliana nasi kwenye makosa kwa uadilifu, hivyo basi akafanya malipo ya kosa moja ni moja hivyo hivyo.
  3. Ukubwa wa dhambi ya kumshirikisha Mwenyezi Mungu, katika hilo kunapelekea kuharamishiwa kuingia peponi.
  4. Kumewekwa wazi utukufu na ubora wa kutoa katika njia ya Mwenyezi Mungu.
  5. Ongozeko la thawabu za kutoa katika njia ya Mwenyezi Mungu, linaanzia ziada ya mia saba; Kwa sababu kutoa kunasaidia kuliinua neno la Mwenyezi Mungu.
  6. Kumewekwa wazi aina za watu na tofauti zao.
  7. Mwenyezi Mungu humkunjulia muumini na asiyekuwa mumini hapa Duniani, na wala hamkunjulii Akhera isipokuwa muumini tu.