عَن أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«يَأْتِي الشَّيْطَانُ أَحَدَكُمْ فَيَقُولُ: مَنْ خَلَقَ كَذَا؟ مَنْ خَلَقَ كَذَا؟ حَتَّى يَقُولَ: مَنْ خَلَقَ رَبَّكَ؟ فَإِذَا بَلَغَهُ فَلْيَسْتَعِذْ بِاللهِ وَلْيَنْتَهِ».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 3276]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake-:
Shetani humjia mmoja wenu na akamwambia: Ni nani aliumba kitu fulani? Mpaka anafikia kusema ni nani alimuumba Mola wako? Basi ikiwa atafikia kuuliza hivyo basi na ajikinge kwa Mwenyezi Mungu na awache kuuliza maswali hayo."
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 3276]
Anaeleza Mtume Rehema na amani ziwe juu yake- kuhusu tiba sahihi ya kujiepusha na maswali ambayo Shetani huyatumia kumtia wasiwasi muumini, Basi Shetani husema: Ni nani aliyeumba kitu fulani? Ni nani aliyeumba mbingu? Ni nani aliyeumba Ardhi? Hivyo basi muumini kutokana na dini yake na maumbile yake na akili yake humjibu kwa kusema kuwa ni Mwenyezi Mungu, Lakini Shetani haishii hapo kwenye kutia wasiwasi, bali anahama mpaka anafikia kusema; Ni nani aliyemuumba Mola wako? Basi wakati huo muislamu atajizuilia na wasiwasi huu kwa kufanya mambo matatu:
Kwa kumuamini Mwenyezi Mungu.
Na kwa kujikinga kwa Mwenyezi Mungu kutokana na Shetani,
Na kuacha kuendekeza wasiwasi.