Orodha ya Hadithi

Dhikiri bora ni: Laa ilaaha Illa llaah: Na dua bora ni: Al-hamdulillah
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Palipo karibu zaidi kwa mja na Mola wake ni pale anapokuwa kasujudu,Basi zidisheni dua
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Maneno yanayopendeka zaidi kwa Allah ni manne: Sub-haanallah, Al-hamdulillaah, na Laa ilaaha illa llaah, na Allahu Akbar, haidhuru ikiwa utaanza na lolote kati ya hao
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Maneno mawili mepesi mno katika ulimi, ni mazito mno katika mizani, yanapendeka mno kwa Al-Rahmani (Mwingi wa rehema)
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Atakayeshuka mahali akasema: Audhubikalimaatillaahit-taammaati min sharri maa khalaqa (Najilinda kwa maneno ya Mwenyezi Mungu yaliyotimia kutokana na shari ya vile alivyoviumba) hakitomdhuru kitu mpaka aondoke mahala pake hapo
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Kusema kwangu: Sub-haanallaah, na Alhamdulillaah, na Laa ilaaha illa llaah, na Allaahu Akbaru, kunapendeka sana kwangu kuliko vitu vyote vilizochomozewa na jua
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Atakayesoma aya mbili za mwisho wa suratul Baqara zitamtosheleza
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Twahara ni nusu ya imani, na kusema Al-hamdulillah neno hilo hujaza mizani, na neno Sub-hanallah neno Alhamdulillah maneno hayo mawili hujaza mizani- au hujaza- sehemu iliyopo kati ya Mbingu na Ardhi
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Ewe Abbasi, ewe ami yake na Mjume wa Mwenyezi Mungu, muombe Mwenyezi Mungu afya katika Dunia na Akhera
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Anapoingia mtu nyumbani kwake akamtaja Mwenyezi Mungu wakati wa kuingia kwake na wakati wa chakula chake, Shetani husema: Hakuna malazi kwenu, wala chakula cha usiku
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Alikuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake akisema mara kwa mara: “Ewe Mbadilishaji nyoyo, uweke imara moyo wangu katika dini yako.”
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Msiziombee mabaya nafsi zenu,wala msiwaombee vibaya watoto wenu,wala msiziombee vibaya mali zenu,nakhofia dua hizo zisikutane na muda ambao haombwi Mwenyezi Mungu katika muda huo chochote isipokuwa anakujibuni.
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Hujibiwa mmoja wenu anapokuwa hajafanya haraka: anasema: Nimemuomba Mola wangu, na wala sijaona ananijibu mimi
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Mahala pa karibu zaidi anapokuwa Mola Mlezi na mja ni katikati ya usiku wa mwisho
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Atakayesema: -Yaani: anapotoka nyumbani kwake-: Bismillaahi tawakkaltu a'la llaahi -kwa jina la Mwenyezi Mungu nimemtegemea Mwenyezi Mungu, Laa haulaa walaa quwwata illaa billaa- hakuna ujanja wala nguvu isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu, huambiwa: Umeongozwa na umetoshelezwa na umekingwa, na shetani hujitenga mbali naye
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Hakika mimi ninajua neno ambalo lau kama angelisema yangemuondokea anayaoyapata (katika hasira), lau angesema: Audhubillaahi minash-shaitwani, -Najilinda kwa Mwenyezi Mungu kutokana na Shetani- ingemuondokea hasira anayoipata
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Mimi nipo katika dhana ya mja wangu kwangu, na Mimi nipo naye wakati anaponitaja
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Anafunga shetani juu ya kisogo cha kichwa cha mmoja wenu, pindi anapolala, mafundo matatu, anafunga katika kila fundo usiku kucha na husema : basi lala
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Mfano wa yule anayemtaja Mola wake na yule asiyemtaja Mola wake, ni mfano wa aliyehai na aliyekufa
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Enyi watu! Hakika Mwenyezi Mungu ni mzuri hakubali ila vizuri, na hakika Mwenyezi Mungu amewaamrisha waumini kwa yale aliyowaamrisha kwayo Manabii
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Bahili ni yule ambaye nitatajwa mbele yake, akawa hakuniswalia
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Atakayekula chakula, akasema: Kila sifa njema zinamstahiki Mwenyezi Mungu aliyenilisha chakula hiki, na akaniruzuku, si kwa ujanja wangu wala kwa nguvu zangu, atasamehewa madhambi yake yaliyotangulia
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Dua hairejeshwi (inayoombwa) baina ya adhana na kukimiwa swala
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Ewe Mwenyezi Mungu nitengenezee dini yangu ambayo ndiyo kinga ya jambo langu
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Ewe Mola wangu Mlezi nisamehe mimi makosa yangu, na ujinga wangu, na ubadhirifu wangu katika jambo langu lote, na yale unayoyajua kutoka kwangu, ewe Mola wangu nisamehe makosa yangu, na yale ya makusudi na ujinga wangu na mzaha wangu, na hayo yote yaliyo kwangu, ewe Mola wangu nisamehe niliyoyatanguliza na niliyoyachelewesha, na niliyoyaficha na niliyoyatangaza, wewe ndiye muwahishaji na wewe ndiye mcheleweshaji, na wewe juu ya kila kitu ni muweza
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninakuomba unipe afya katika Dunia na Akhera
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninakuomba (unipe) kutoka katika heri zote: zile za haraka na za kuchelewa, kwa ninayo yajua na nisiyo yajua, na ninajikinga kwako kutokana na shari zote zinazokuja haraka na zinazochelewa
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi najikinga kwako kutokana na kuondokewa neema zako, na kubadilika kwa afya yako, na kufikiwa ghafla na adhabu zako, na kila aina ya hasira zako
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninajikinga kwako kutokana na kushindwa kulipa deni, na kushindwa na maadui, na kutukanwa na maadui
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Ewe Mwenyezi Mungu kwako tumeamka, na kwako tunashinda, na kwako tunakuwa hai, na kwako tutakufa, na kwako tutafufuliwa
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Ilikuwa Dua aiombayo zaidi Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake-:ni "Ewe Mola wetu Mlezi, tupe duniani mazuri, na Akhera mazuri, na utukinge na adhabu ya moto
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Bwana wa Istighfari (Dua ya kuomba msamaha)
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Sema: Ewe Mwenyezi Mungu niongoze na unisimamie, na kumbuka kwa uongofu ni kuongoka kwako njia, na kusimamiwa ni kusimamiwa kupatia (katika kila jambo lako mithili ya) mshale
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Je, nisikujulisheni kitu bora zaidi kuliko hicho mlichoomba? Mtakapokwenda kulala basi msabihini Mwenyezi Mungu; yaani (Sub-haanallaah) mara thelathini na tatu, na mhimidini (Al-hamdulillaah) mara thelathini na tatu, na mtukuzeni (Allahu Akbar) mara thelathini na nne, kufanya hivyo ni bora zaidi kwenu kuliko mfanyakazi.”
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Sema Yeye ni Mwenyezi Mungu mmoja tu" na sura mbili za kinga unapofika nyakati za jioni na nyakati za asubuhi mara tatu, zitakutosheleza kila kitu
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Yeyote atakayesema: Bismillaahi lladhi laa yadhurru ma'asmihi shai un fil Ardhwi walaa fis samaai, wahuwas samiiu'l 'aliim, (Kwa jina la Mwenyezi Mungu ambaye hakuna kinachoweza kudhuru pamoja na jina lake kitu chochote ardhini wala mbinguni, naye ni msikivu na mjuzi) mara tatu, basi halitomfika balaa la ghafla, mpaka atakapoamka
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Sema: Hapana Mola isipokuwa Mwenyezi Mungu yeye pekee asiyekuwa na mshirika, Mwenyezi Mungu mkubwa mno, na kila sifa njema zinamstahiki Mwenyezi Mungu kwa wingi, na ametakasika Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa walimwengu, na hapana ujanja wala nguvu isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu mwenye nguvu na hekima
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Adh-kari za baada ya sala ya faradhi hapati hasara msomaji au mfanyaji wake, kusema Sub-haana llahi mara thelathini na tatu (33), Al-hamdulillahi mara thelethini na tatu (33), Allahu Akbaru mara thelathini na nne (34)
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
alikuwa anapoingia msikitini anasema: "Najilinda kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kwa uso wake mkarimu, na kwa mamlaka yake ya tangu, kutokana na shetani aliyelaaniwa
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Shetani humjia mmoja wenu na akamwambia: Ni nani aliumba kitu fulani? Mpaka anafikia kusema ni nani alimuumba Mola wako? Basi ikiwa atafikia kuuliza hivyo basi na ajikinge kwa Mwenyezi Mungu na awache kuuliza maswali hayo
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Atakapoingia mmoja wenu msikitini basi aseme: Allaahummaf-tah lii abwaaba rahmatika (Ewe Mola wangu, nifungulie milango ya rehema zako), na akitoka aseme: Allaahumma innii as-aluka min fadhlika (Ewe Mola wangu ninakuomba unipe katika fadhila zako)
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Huyo ni Shetani anaitwa Khinzab, ukimuhisi basi haraka sana taka ulinzi kutoka kwa Allah dhidi yake, na uteme kushotoni kwako mara tatu
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Ewe Mwenyezi Mungu kwa ajili yako nimejisalimisha, na kwako nimeamini, na juu yako nimetegemea, na kwako nimejisogeza, na kwa ajili yako napambana. Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi najikinga kwako kwa utukufu wako hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa wewe najikinga kwa kuto nipoteza, wewe ndiye uliye hai ambaye hafi, na majini na watu wanakufa
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi nakuomba uongofu na uchamungu na kujizuia na machafu nakuwa ni mwenye kutosheka
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Atakayesema: Sub-haanallaahi wabihamdi, (Ametakasika Mwenyezi Mungu Mtukufu na sifa njema ni zake) ataoteshewa mti wa mtende peponi
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Enyi watu, tubieni kwa Mwenyezi Mungu, kwani mimi ninatubia kwa siku mara mia moja
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Hakuna muislamu yeyote ataomba maombi yasiyokuwa ndani yake na kuomba dhambi wala kukata udugu, isipokuwa Allah atampa kwa maombi hayo moja kati ya mambo matatu: Moja ima amuharakishie maombi yake, au amlimbikizie ili amlipe siku ya Kiyama, au amuondoshee katika mabaya mfano wake" Wakasema: (Maswahaba) kwa hiyo tuzidishe? Akasema: "Allah ni mwenye kuzidisha mara dufu
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- alikuwa akisema wakati wa matatizo: "Laa ilaaha illa llaahul a'dhwiimul haliim, Laa ilaaha illa llaahu Rabbul A'rshil A'dhwiim, Laa ilaaha illa llaahu Rabbu ssamaawaati warabbul A'rshil kariim" Tafsiri: Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu na Mpole, Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu Mola wa A'rshi tukufu, Hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu Mola wa mbingu, na Mola wa ardhi, na Mola wa A'rshi takatifu
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- alikuwa akisema katika sijida yake: "Ewe Mwenyezi Mungu nisamehe mimi dhambi zangu ndogo zake na kubwa zake za mwanzo wake na mwisho wake, za wazi zake na za siri zake
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Hakika Mola wenu Mlezi ni Mwenye haya Mkarimu, anamuonea haya mja wake atakapo nyanyua mikono yake kumuelekezea kisha amrejeshe patupu
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Hakika ungesema maneno manne, mara tatu, kama ungeyapima kwa uliyo yasema toka siku ya leo yangeyazidi uzito
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Hawajawahi kukaa watu kikao chochote wakawa hawakumtaja Mwenyezi Mungu ndani yake, na wala hawakumsalia Nabii wao, isipokuwa itakuwa ni hasara juu yao, akitaka atawaadhibu na akitaka atawasamehe
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akipendelea dua fupi yenye kukusanya, na anaacha mengine yasiyokuwa hiyo
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Msiutukane upepo, mkiona yanayo kuchukizeni katika upepo basi semeni: Ewe Allah tunaomba kheri za upepo huu na kheri zilizomo, na kheri ambazo kwazo umeamrishwa upepo huu, na tunataka hifadhi na ulinzi kutokana na shari zake ,na shari ambazo kwa sababu yake umeamrishwa
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Asiseme mmoja wenu: Ewe Mwenyzi Mungu nisamehe ukitaka, nirehemu ukitaka, niruzukua ukitaka, na adhamirie maombi yake, kwani yeye anafanya ayatakayo, hakuna wa kumlazimisha
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Amepata hasara mtu nitakayetajwa mbele yake na akawa hakunitakia rehema, na kapata hasara mtu ambaye itaingia Ramadhani mpaka ikatoweka kabla hajasamehewa, na kapata hasara mtu atakayewapata wazazi wake akiwa mtu mzima na wao wakiwa wazee na wakawa hawakumuingiza peponi
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Hakika nyoyo za wanadamu zote ziko baina ya vidole viwili miongoni mwa vidole vya Rahmaan (Mwingi wa rehema), kama moyo wa mtu mmoja, anaugeuza kokote atakako
عربي Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu
Mkimuomba Allah basi muombeni Firdausi
عربي Lugha ya Kiindonesia Kisin-hala
Atakayesema nimeridhia Mwenyezi Mungu kuwa Mola, na kuwa Uislamu ni dini, na Muhammadi kuwa Mtume, basi atastahiki kwake Papo
عربي Lugha ya Kiindonesia Kisin-hala
Watu wa aina saba atawapa kivuli Mwenyezi Mungu Mtukufu siku ambayo hapatokuwa na kivuli isipokuwa kivuli chake
عربي Lugha ya Kiindonesia Kisin-hala