عَنْ عَائِشَةَ رضي الله عنها قَالَتْ:
كَانَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَسْتَحِبُّ الْجَوَامِعَ مِنَ الدُّعَاءِ، وَيَدَعُ مَا سِوَى ذَلِكَ.
[صحيح] - [رواه أبو داود وأحمد] - [سنن أبي داود: 1482]
المزيــد ...
Kutoka kwa Aisha -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema:
Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akipendelea dua fupi yenye kukusanya, na anaacha mengine yasiyokuwa hiyo.
[Sahihi] - - [سنن أبي داود - 1482]
Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akipendelea dua zenye kukusanya kheri za dunia na Akhera ambazo matamshi yake ni machache na maana yake ni nyingi, na kunakuwa ndani yake na kumtukuza Mwenyezi Mungu Mtukufu, na malengo mazuri, na anaachana na yasiyokuwa hayo.