عَنْ عَلِيٍّ رَضيَ اللهُ عنهُ أَنَّ مُكَاتَبًا جَاءَهُ، فَقَالَ: إِنِّي قَدْ عَجَزْتُ عَنْ مُكَاتَبَتِي فَأَعِنِّي، قَالَ: أَلاَ أُعَلِّمُكَ كَلِمَاتٍ عَلَّمَنِيهِنَّ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ، لَوْ كَانَ عَلَيْكَ مِثْلُ جَبَلِ صِيرٍ دَيْنًا أَدَّاهُ اللَّهُ عَنْكَ، قَالَ:
«قُلْ: اللَّهُمَّ اكْفِنِي بِحَلاَلِكَ عَنْ حَرَامِكَ، وَأَغْنِنِي بِفَضْلِكَ عَمَّنْ سِوَاكَ».
[حسن] - [رواه الترمذي] - [سنن الترمذي: 3563]
المزيــد ...
Kutoka kwa Ally radhi za Allah ziwe juu yake ya kwamba mtu mmoja aliyeandikishana kujitoa katika utumwa alimjia akasema: Hakika mimi nimeshindwa kulipa deni tuliloandikishana, basi naomba unisaidie, akasema: Je, nikufundishe maneno ambayo alinifundisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake, hata kungekuwa juu yako na deni zito mfano wa mlima Swiri Mwenyezi Mungu atakulipia, akasema:
"Sema: Allaahumma kfinii bihalaalika an haraamika, wa aghninii bifadhlika amman siwaaka". Tafsiri: Ewe Mwenyezi Mungu nitosheleze kwa halali yako dhidi ya haramu yako, na unitajirishe kwa fadhila zako nisimuhitaji yeyote asiyekuwa wewe.
[Ni nzuri] - [Imepokelewa na Imamu Tirmidhiy - Imepokelewa na Ahmad] - [سنن الترمذي - 3563]
Alimuijia kiongozi wa waumini Ally bin Abii Twalib radhi za Allah ziwe juu yake bwana mmoja mtumwa alikuwa kaandikishana na bwana yake na amekubaliana naye ili aikomboe nafsi yake na aiache huru ili awe huru, na hakuwa na mali, akasema: Hakika mimi nimeshindwa kulipa deni hilo juu yangu, nakuomba unisaidie kulilipa kwa mali, au kwa kunifundisha na kunielekeza, akasema kumwambia kiongozi wa waumini: Je, nikufundishe maneno aliyonifundisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake, lau kama ungelikuwa na deni mfano wa mlima Swiri wa kabila la Twayyi basi Mwenyezi Mungu angelikulipia kwa mstahiki wake, na angelikuokoa kutoka katika madhila yake, akasema: Sema: "Ewe Mwenyezi Mungu nitosheleze" na uniepushe na uniweke mbali "kwa halali yako" nitosheke nayo "dhidi ya" kutumbukia katika "haramu yako", na unitosheleze "kwa fadhila zako" na ukarimu wako "kutomuhitaji yeyote" katika viumbe.