عَنْ زَيْدِ بْنِ أَرْقَمَ رَضيَ اللهُ عنه قَالَ: لَا أَقُولُ لَكُمْ إِلَّا كَمَا كَانَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ: كَانَ يَقُولُ:
«اللهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنَ الْعَجْزِ وَالْكَسَلِ وَالْجُبْنِ وَالْبُخْلِ وَالْهَرَمِ وَعَذَابِ الْقَبْرِ، اللهُمَّ آتِ نَفْسِي تَقْوَاهَا، وَزَكِّهَا أَنْتَ خَيْرُ مَنْ زَكَّاهَا، أَنْتَ وَلِيُّهَا وَمَوْلَاهَا، اللهُمَّ إِنِّي أَعُوذُ بِكَ مِنْ عِلْمٍ لَا يَنْفَعُ، وَمِنْ قَلْبٍ لَا يَخْشَعُ، وَمِنْ نَفْسٍ لَا تَشْبَعُ، وَمِنْ دَعْوَةٍ لَا يُسْتَجَابُ لَهَا».
[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 2722]
المزيــد ...
Kutoka kwa Zaidi bin Arqam radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Sikwambieni isipokuwa kama alivyokuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema: Alikuwa akisema:
"Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi najikinga kwako kutokana na kushindwa, na uvivu, na uoga, na ubahili, na ukongwe, na adhabu ya kaburi, Ewe Mwenyezi Mungu ipe nafsi yangu uchamungu wake, na uitakase kwani wewe ndiye mbora wa kuitakasa, wewe ndiye msimamizi wa nafsi na mtawala wake. Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninajikinga kwako kutokana na elimu isiyo na manufaa, na moyo usiyo nyenyekea, na nafsi isiyo tosheka, na maombi yasiyo jibiwa".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 2722]
Ilikuwa katika dua za Mtume rehema na amani ziwe juu yake: "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninajikinga kwako" na ninajiegemeza kwako, "Kutokana na kushindwa" kwa kukosa uwezo wa unjanja wenye manufaa, "na uvivu" kwa kushindwa kuendesha mambo, aliyeshindwa hana ujanja, na mvivu hana haja nao, "na uoga" kwa kujizuia kuyaendea yanayopasa kufanywa, "na ubahili" kwa kuzuia yanayopaswa kuyatoa, "na ukongwe" na ukubwa wa umri unaopelekea udhaifu wa mwili, "na adhabu za kaburi" na sababu zinazopelekea katika hayo. "Ewe Mwenyezi Mungu ipe nafsi yangu" na uipe na uiwezeshe katika "uchamungu wake" kwa kufanya uchamungu na kuacha maasi, "na uitakase" na uisafishe kutokana na uchafu na tabia mbaya, "wewe ndiye mbora wa kuitakasa" na wala hakuna wa kuitakasa yeyote zaidi yako, "Wewe ndiye msimamizi wake" na mtetezi wake na msimamizi wake, "na Mola wake" Msimamizi wa mambo yake, na Mola wake Mlezi na mwenye kuineemesha. "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi ninajikinga kwako kutokana na elimu isiyokuwa na manufaa", kama elimu ya nyota na ukuhani na uchawi, au isiyo na manufaa Akhera, au elimu isiyofanyiwa kazi, "na moyo usionyenyekea" kwako, na wala haujishushi, na wala hautulii, wala hautulizani kwa kukutaja, "na nafsi isiyoshiba" wala isiyokinai kwa yale iliyopewa na Mwenyezi Mungu na akairuzuku miongoni mwa halali nzuri, "na kutokana na maombi" yenye kurudishwa "yasiyopokelewa".