عن أنس بن مالك رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه وسلم قال:
«يَسِّرُوا وَلَا تُعَسِّرُوا، وَبَشِّرُوا وَلَا تُنَفِّرُوا».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 69]
المزيــد ...
Kutoka kwa Anasi bin Maliki -Radhi za Allah ziwe juu yake- kutoka kwa Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- amesema:
"Fanyeni mambo kuwa mepesi na wala msiyafanye kuwa magumu, na wapeni watu bishara njema na wala msiwakimbize".
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 69]
Anaamrisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwafanyia wepesi watu na kutowafanyia ugumu katika mambo yote ya Dunia na Akhera, na hili liwe katika mipaka aliyoihalalisha Mwenyezi Mungu na sheria.
Na anahimiza kuwapa bishara kwa kheri, na kutowakimbiza.